Na Mussa Augustine
Jeshi la zimamoto na Uokoaji Mkoa wa zima Moto Ilala limeishauri Halmashauri ya Jiji la Ilala kuhakikisha inatenga
Miundombinu ya barabara ili kuweza kurahisisha kufika kwenye eneo ambapo ajali ya Moto ilipotokea na kuweza kuudhiti.
Pia limesema kuwa limekuwa linapata changamoto ya kukosa maji baada ya maji yanayokuwepo kwenye magari ya Zima Moto kuisha wakati wa kuzima moto hali ambayo inatokana na kukosekana Kwa visima Maalumu vya maji Kwa ajili ya kazi ya hiyo katika maeneo mbalimbali Jijini humo.
Hayo yamesemwa Januari juzi na Mrakibu Wa Zima Moto na Uokoaji Elisa Mugisha ambaye ni Kamanda wa Jeshi la zima Moto na Uokoaji Mkoa wa Zima Moto Ilala.
Aidha Kamanda Mugisha amesema Jeshi hilo limekua likilalamikiwa Kwamba linachelewa kufika katika eneo la tukio kuzima moto unapotokea lakini akafafanua kuwa hali hiyo inatokana na kukosekana Kwa barabara zinazopitika Kwa urahisi kutokana na hali ya mipango miji ilivyo.
“Sisi Jehi la zima Moto na Uokoaji tunalaumiwa sana kwamba tunachelewa kufika kwenye eneo la tukio kudhibiti moto nakufanya Uokoaji ,ukweli nikwamba wakati mwingine tunachelewa kupata taarifa kutoka kwa wananchi,lakini pia hua kuna foleni ya magari Barabarani au kukosekana kabisa Kwa barabara eneo hilo” amesema.
Nakuongeza kuwa” Halmashauri za Wilaya na Majiji zinapaswa kuweka visima vya maji ili tunapozima moto halafu maji yanaisha tunapata maji mengine Kwa haraka hii inatusaidia kudhibiti moto haraka ,pia wananchi wapaswa kutoa taarifa Kwa namba ya msaada 114 ” amesema.
“Halmashauri za Wilaya Majiji zinatakiwa kuzingatia sheria Kwa kufuata Michoro,Ujenzi na Matumizi ya Miundombinu iliyoelekezwa kwenye ramani ya mipango miji (Master Plan).” Amesema Kamanda Mugisha.
Aidha ameongeza kuwa Jeshi hilo la zima Moto na Uokoaji limekua likifanya Mafunzo yakujiweka tayari kukabiliana na Mioto muda wote,nakwamba kwenye maeneo ya soko na mashuleni Jeshi hilo linaendelea kutoa elimu ya namna ya kujikinga na ajali za moto.