Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema wanajeshi wake wanatimiza malengo yao kufuatia mashambulizi katika eneo la Urusi la Kursk, yaliyoanzishwa karibu wiki mbili zilizopita.

Kwenye hotuba yake, Zelensky amesema “nimepokea ripoti kutoka kwa Kamanda Mkuu wa jeshi Syrskyi kuhusu hali ya mashariki mwa Ukraine na operesheni katika eneo la Kursk. Wanajeshi wetu wanafanya vizuri kila sehemu. Lakini kuna haja ya kuwasilisha haraka vifaa kutoka kwa washirika wetu. Hakuna likizo wakati wa vita. Hatua zinapaswa kuchukuliwa na ninaziomba Marekani, Uingereza na Ufaransa kuwezesha upatikanaji wa misaada zaidi.”

Serikali mjini Kyiv imesema uvamizi huo katika ardhi ya Urusi una lengo la kuilinda Ukraine na pia kuilazimisha Urusi kuja kwenye meza ya mazungumzo kwa masharti ya haki.

Hata hivyo, Urusi ambayo imedai kuchukua udhibiti wa mji wa Zalizne huko Donetsk, imesema mashambulizi ya Kursk yanamaanisha kwamba kwa sasa hakutokuwepo mazungumzo yoyote ya amani na Ukraine.

Watu zaidi ya 120,000 wamehamishwa huko Kursk kufuatia mashambulizi ya Ukraine.

Please follow and like us:
Pin Share