TIMU ya wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Zambia, imefanya ziara ya mafunzo katika Wizara ya Fedha Tanzania.

Lengo la mafunzo ni lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya uendeshaji ikiwemo usimamizi wa madeni ya ndani.

Mafunzo hayo yamefanyika Ofisi za Wizara ya Fedha jijini Dodoma.

Yameshirikika timu hiyo kutoka Zambia ikioongozwa na Mkurugenzi Msaidizi Uwekezaji na Usimamizi wa Madeni, Wizara ya Fedha na Mipango Zambia, Patrick Mfungo na upande wa Tanzania ukioongozwa na Kamishna Msaidizi Idara ya Madeni, Wizara ya Fedha, Nuru Ndile.