China kuifufua Tazara, Kikwete Mwenyekiti

Machi 23, mwaka huu, Rais Kikwete ameupokea ujumbe wa Serikali ya China unaotaka kuifufua reli hii. Kikwete amekubali kuwa Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya kuifufua Taaara na kamati hii sasa taarifa zilizopo ni kama imeshaanza kazi.

Wiki iliyopita, uongozi wa juu wa Tazara ulikuwa safarini nchini Zambia, kufanya kikao cha jinsi ya kuboresha huduma za reli hii. Ndumbalo ameithibitishia JAMHURI kufanyika kwa ziara hii.

Taarifa zilizoifikia JAMHURI zinaonyesha kuwa China katika kuifufua reli hiyo imepanga kutoa mabehewa mapya 40, injini 10 za treni, injini nne za kuhamisha mabehewa, vifaa mbalimbali vya kukarabati reli iliyopo na winchi moja.

Matumaini ya China ni kwamba vifaa hivyo vitaifanya Tazara kurejea katika hali yake ya zamani, na kuwa mtambo wa kuzalisha fedha.

Je, Rais Kikwete atakubali aibu ya Tazara kwa kuruhusu imfie mikononi mwake? Je, Kikwete atakubali kuendelea na mameneja ambao hawaagizi mafuta hadi treni inazimikia njiani? Na je, Mamlaka itaendelea na Sheria hii ya mwaka 1975 inayofunga mikono kuhusu biashara hadi lini?

Gazeti la JAMHURI linasema ni ama wahusika wote wakubali kubadilika au vinginevyo watakumbwa na tsunami ya mabadiliko ya kiuchumi duniani. Timizi wajibu wako.