Mabehewa yauzwa DRC
Wafanyakazi wameijulisha JAMHURI kuwa baadhi ya mabehewa yameibwa au yamepelekwa kinyemela nchini DRC, na kwamba malalamiko hayo wameyafikisha rasmi kwa Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu.
JAMHURI imejitahidi kwa kila hali kuwasiliana na Waziri Nundu, lakini wakati wote simu yake inaita bila kupokewa. Ila awali Ndumbalo aliliambia gazeti la JAMHURI kuwa maneno hayo ni uzushi. Hakuna behewa wala injini ya treni iliyopataka kuibwa.
“Sishangai tuhuma kama hizo kutolewa, hata mimi nimezisikia na kuzichunguza. Ninachoweza kusema ni kuwa hakuna kichwa cha treni kilichouzwa wala kuondoka kwenye reli ya Tazara. Ukweli ni kwamba kuna kichwa kimoja ndiyo kime… kina namba 1003 ambacho kimepata ajali mara mbili na kupata ufa.
“Mafundi walikwishaingiza hata imani za ushirikina, wakakichinjia hadi mbuzi…lakini walileta gharama za matengenezo zipatazo Sh milioni 45. Hapo katikati tukapata kampuni kutoka Congo, iliyokuwa tayari kukodisha hiyo injini, kuitengezesha na kuendelea kutulipa, ikakwamishwa. Matokeo yake mafundi wetu wakaifungua ipo pale Mbeya.
“Katika kutengeneza hiyo injini kwa gharama ya Sh milioni 45, waliweka posho zao Sh milioni 30. Ina maana hii injini itengenezwe kwa Sh milioni 75. Kelele hizi unazosikia zinaanzia hapo.
“Kwamba tumesimamisha malipo na utengenezaji umesimama. Kwa kuwa hawapati hizo fedha wanachochea wenzao. Nimemuuliza Chief Mechanical Engineer anasema imeshushwa chini na ipo pale Mbeya,” amesema Ndumbalo.