Mbao, saruji vyapungua Tazara

Taarifa za chini chini zinasema aina ya mkataba wa kuanzishwa kwa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia, ndiyo chimbuko la mgogoro wote uliopo.

Inaelezwa kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu kutoka Tanzania hata kama angekuwa na nia njema kiasi gani, hawezi kufanya lolote kwani mweye mamlaka ya mwisho katika kuamua nini kinapaswa kufanywa ndani ya Tazara ni Mzambia kwa mujibu wa Taara Act, 1975.

Baadhi ya wafanyakazi wameiambia JAMHURI kuwa wakurugenzi kutoka Zambia wanapandisha bei za mizigo kwa makusudi, kwa matumaini kuwa Watanzania watashindwa kuendelea kuitumia reli hiyo, ili wao pekee waendelee kuitumia kusafirishia shaba.

Si hilo tu, zipo hisia zilizoelezwa na wafanyakazi kuwa Wazambia wanahujumu utendaji wa Tazara kwa makusudi kwa kukwamisha uchumi wa Tanzania kama taifa lisiwapite, kwani wakiangalia mzigo unaosafirishwa kutoka mikoa ya kusini na nchi jirani, inawatia hofu kuwa taifa hili litatajirika haraka na wao watabaki kuwa tegemezi kwa Tanzania, kitu wasichotaka kitokee.