Na Happy Lazaro, JamhuriMedia, Arusha

Zaidi ya wanawake mia sita kutoka mikoa saba wanatarajiwa kujengewa uwezo kuhusu maswala ya uongozi na ushiriki wa wanawake katika kufanya maamuzi .

Hayo yamesemwa mkoani Arusha na mwezeshaji kutoka idara ya sayansi ya siasa na utawala kutoka chuo kikuu cha DSM ,Prof.Bernadeta Killian wakati akizungumza katika mafunzo ya uongozi wa mabadiliko kwa ajili ya wanawake viongozi kwenye ngazi ya Serikali za Mitaa yaliyofanyika mkoani Arusha .

Mwezeshaji kutoka Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala kutoka chuo kikuu cha DSM ,Prof.Bernadeta Killian wakati akizungumza katika mafunzo hayo mkoani Arusha

Amesema kuwa,wanatoa mafunzo kwa viongozi wakiwemo madiwani waliochaguliwa, madiwani wa viti maalum,wenyeviti wa serikali za mitaa na wenyeviti wa serikali ya kijiji ,pamoja na wenyeviti wa majukwaa mbalimbali mkoani Arusha .

Ameongeza kuwa ,kwa hapa Arusha wanatoa mafunzo kwa wanawake 90 kwa ujumla ambapo wakitoka hapo wataenda wilayani Karatu ambapo lengo la kutoa mafunzo hayo ni kujenga uwezo wa wanawake kama viongozi na kuwa viongozi katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Amesema kuwa, wanatoa mafunzo hayo kwenye mikoa saba ambapo hadi sasa hivi wameshatoa mafunzo hayo katika mkoa wa Dar es Salaam,Tanga, Pwani,Singida,Mtwara, Lindi, na Arusha ambapo wakitoka hapo hapo wanaenda mkoa wa Kigoma .

Washiriki mbalimbali wakifuatilia mada mbalimbali katika mkutano huo mkoani Arusha

Amefafanua zaidi kuwa ,mradi huo.kwa ujumla unafadhuliwa na shirika la Un Women Tanzania ikishirikiana na serikali ya Finland ambapo unaendeshwa katika ngazi ya Tamisemi .

Ameongeza kuwa,mafunzo hayo waliyafanya 2017 hadi 2020 mradi ukaisha ndo wakapata huo.ufadhili ambapo utofauti wa sasa ni kuwa Un Women imeingia makubaliano na mashirikiano na serikali katika ngazi ya mkoa na halmashauri ambapo unasimamiwa moja kwa moja na serikali za mkoa na serikali za mitaa (TAMISEMI).

“Tunafanya kazi kwa karibu kabisa na maafisa maendeleo ya jamii ambao wapo katika ngazi mbalimbali kwani ndio ambao wanatusaidia kutafuta washiriki wanaostahiki kuingia kwenye hayo mafunzo .”amesema.

Ameongeza kuwa mafunzo hayo walianza mwaka jana na hivyo ni muhimu kwani ushiriki wa wanwake katika kufanya maamuzi ni mdogo hivyo mafunzo hayo yanatumika kujengea uwezo wanawake ili tuweze kuongeza idadi yao katika vyombo mbalimbali vya kufanya maamuzi kwa kupitia uchaguzi.

Kwa upande wake Afisa maendeleo ya jamii mkoa Arusha ,Blandina Nkini amesema kuwa, tangu mafunzo hayo yaanze kutolewa wameona mabadiliko makubwa sana hasa kwa zile kata zenye mradi kwani wakina mama wamekuwa na mwamko mkubwa katika kugombea nafasi mbalimbali.

Naye Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake kata ya Muriet, Miriam Mbise maarufu kama “mama Simanjiro”, amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kwa kiasi kikubwa kuwakumbusha wajibu wao na kuwa na udhubutu katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi .