Timu ya Yanga imeshinwa kuutumia vema uwanja wake wa nyumbani kwenye michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika, baada ya kutoka sare tasa ya bila kufungana na Rayon Sports ya Rwanda
Katika mchezo huo ambao ulipigwa kwenye dimba la Taifa, Yanga watajiraumu wenyewe baada ya kukosa nafasi nyingi za wazi.
Kwa upande wa Rayon Sports wamepoteza nafasi mbili ambazo walifunga mabao mawili lakini yote yalikataliwa na muamuzi kutokana wachezaji waliofunga walikuwa offside.
Matokeo ya Mechi nyingine katika kundi hilo ni Gor Mahia ya Kenya imetoka sare ya bila kufungana na USM Alger ya Algeria.
Kwa matokeo hayo Yanga inaburuza mkia katika kundi lao wakiwa na point moja huku Rayon wakiwa na point 2, sawa na Gor Mahia nao wana point 2 na USM Alger wanaongoza kundi hilo kwa kufikisha poimt 4.
Mechi zinazofuata Yanga watacheza na Gor Mahia na Rayon Sports itacheza na USM Alger.