Timu ya Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Red Arrows ya Zambia katika mchezo wa kirafiki wa kuhitimisha Tamasha la Kilele ya wiki ya Mwananchi katika mchezo uliopigwa Agosti 4, 2024 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Red Arrows ni mabigwa wa mwaka klabu Bigwa Afrika Mashariki na Kati walitangulia kupata bao kupitia mshambuliaji wao Ricky Banda Dakika ya Sita ya mchezo huo.

Dakika ya 62 mzawa Mudathir Yahya Abbas alisawazisha, huku Stephane Aziz Ki akiipatia ushindi timu yake Dakika ya 90+ 3 kupitia mkwaju wa penati.

Baada ya mchezo huo Yangu inatarajiwa  kurejea kambini Avic Town, Kigamboni, Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba Sc utakaopigwa Agosti 8, 2024 katika Dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Please follow and like us:
Pin Share