Mabingwa Watetezi, Yanga SCĀ  imefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 8 -1 dhidi ya Stand United katika mchezo uliochezwa leo Aprili 15, 2025 katika Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.

Mabao ya Yanga yamefungwa na kiungo wa Kimataifa wa Burkina Faso Stephane Azizi Ki ambapo amefunga mabao manne dakika ya 10, 48, 58 na 61 huku akiwasaidia benki Nickson Kibabage na kiungo Mzambia Clatous Chama mabao mawili dakika ya 32 na 40.

Bao la nane la Yanga limefungwa na Mshambuliaji Mzambia Kennedy Msonda, huku bao pekee la Stand United likifungwa na Msenda Senda dakika ya 48.