Klabu ya Yanga imemtaka mchezaji wake Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ kuripoti kambini haraka iwezekanavyo mara baada ya klabu hiyo kupokea marejeo ya Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji kuhusu suala la mchezaji.
Hayo yamesema kupitia taarifai liyotolewa na klabu hiyo Machi 6, 2023
“Baada ya kupokea maamuzi hayo, Klabu ya Yang imemwandikia barua Feisal Salum kumtaka aripoti kambini haraka iwezekanavvo na kuendelea kuutumikia mkataba wake kama mchezaii halali wa Yanga mpaka tarehe 30, Mei 2024, kama ilivyoamuliwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF.”imesema taarifa hiyo
Aidha, Klabu ya Yanga iko tayari kumpokea Feisal Salum na kumjumuisha kwenye kikosi, na kwa kuzingatia sera na utaratibu wa Klabu ya Yanga katika kuwaongezea mikataba wachezai wake wanaofanya vizuri, Uongozi wa Yanga uko tayari kuendelea na mazungumzo na Feisal Salum Abdallah na wawakilishi wake juu ya kuboresha mkataba wake, kama wataridhia.
Mwisho, Klabu ya Yanga inapenda kuutaarifu umma kwamba iko tavari kumruhusu Feisal Salum Abdallah kuondoka klabuni kwa kuzingatia matakwa ya mkataba na utaratibu wa sheria za uhamisho wa wachezait zinazotambulika na TFF pamoja na FIFA. Ikiwa pia kuna klabu yoyote inahitaji huduma ya mchezaji huyu, klabu ya Yanga iko tayari kufanya mazungumzo wakati wowote.