Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Pwani

Shirika la Uhifadhi wa Mazingira na Wanyamapori (WWF) ,limewataka Waandishi wa habari Bara na Visiwani ,kutumia kalamu zao kutoa elimu kwa jamii juu ya mkataba wa Kimataifa wa Biashara ya Wanyamapori, Mimea iliyo hatarini kutoweka (CITES) kwa maendeleo endelevu ya viumbe hai.

Rai hiyo imetolewa Ofisa Sera na Uchechemuzi Moureen Mboka wa WWF ,kwenye mkutano na waandishi wa habari ulifofanyika Kibaha mkoani Pwani .

Moreen amesema lengo kuu la warsha hiyo ya siku mbili, kwa Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali Bara na Visiwani ni kuwajengea uwezo juu ya umuhimu wa mkataba wa CITES kwa viumbe hai na mimea.

Amesema lengo kuu la WWF ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari ,ili wawe chachu ya kueneza elimu kwa jamii waweze kutunza viumbe hai na mimea iliyo hatarini kutoweka kwa maendeleo endelevu.

“WWF imeamua kutumia Waandishi wa habari kwasababu wao wana nguvu kubwa katika jamii ,hivyo wakifundishwa vizuri na kupata uelewa juu ya mkataba wa CITES wataweza kutumia kalamu zao kusadia Wananchi kufahamu namna unavyofanya kazi lakini pia Serikali kutokomeza biashara haramu ya Wanyamapori”Amesema.

Ameongeza kuwa kupitia warsha hiyo Waandishi wametoa maoni yao juu ya uenezaji elimu kwa jamii, ambayo wameyajumuisha katika mkakati wa pamoja wa utekekelezaji wa mkataba huo kupitia vyombo vyao.

“Elimu hii ikisambazwa katika jamii itasadia Serikali kuokoa Bioanuwai, ambazo ziko hatarini kutoweka na ambazo hazitakiwi kuuzwa kwa mujibu wa mkataba “amesema Moureen..

Mmoja wa waandishi Kunda Erick amesema warsha hiyo ni muhimu kwa Waandishi wa habari ,kwasababu imewasadia kuwajengea uwezo juu ya namna gani mkataba wa CITES , unavyofanya kazi ili iwe rahisi kwao kutumia kalamu zao kutoa elimu kwa jamii kwa kuandika habari mbalimbali zitakazo saidia kupambana na biashara haramu ya viumbe pori na mimea.

“Kama waandishi tuna jukumu la kusadia kueneza uelewa wa mkataba huu kwenye jamii, ili waweze kulinda wanyamapoli na mimea iliyohataini kutoweka katika maeneo yao”Amesema.

Mwezeshaji wa warsha hiyo Steven Kapinga amesema lengo la kuwakutanisha, Waandishi kwa pamoja ni kuwajengea uwezo na kujadili kwa undani changamoto zilizopo kwenye jamii zinazozuia utekelezaji wa mkataba huo ili wakapaze sauti kupitia kalamu zao mwishowe viumbe hai na mimea viwe salama na dumivu

“Matumaini yetu baada ya mkutano watakwenda kuwa wajumbe katika vyombo vyao , hasa wakati wa kutekelezaji wa utoaji elimu ya mkataba kwenye jamii pia maoni yao waliokusanya yatakwenda kufanyiwa kazi na kuona Waandishi wanashiriki kwenye utekelezaji wa mkataba kwa kutumia kalamu zao

Tunatarajia jamii kuwa na uelewa kuhusu mwenendo wa mkataba, pia watakuwa na ushiriki imara na thabiti wa kutoa maoni yao na kwenye utekelezaji wa sera’amesema.

Mkataba wa CITES umeweka mfumo wa utoaji maamuzi kuhusu utekelezaji wa mkataba kuanzia ngazi ya kamati za kitaalam, kamati kuu na mkutano mkuu wa wanachama conference of parties

Warsha itawasadia Waandishi na Wananchi , kutambua mazao ya misitu na Wanyamapori ambayo hayaruhusiwi kufanyiwa biashara kimataifa na masharti maalumu ambayo yanawekwa kwa mujibu wa mkataba wa CITES kwa ajili ya kuwezesha biashara ya Wanyamapori

Nukuu kwenye Sera ya Wanyamapori ,Mwaka 1961 wakati wa hayati Mwalimu J.K. Nyerere kwenye Azimio la Arusha, limekuwa likitumika kutoa mwongozo wa kuhifadhi wa Wanyamapori katika Tanzania hadi hivi leo.

Katika muda wote huo, Wanyamapori walikuwa wakilindwa na kutumiwa kwa kufuata maelekezo, kanuni na sheria zilizokuwa zikitumiwa.

Kipindi hicho Tanzania ilikuwa na idadi kidogo ya watu (milioni 8 tu), idadi ambayo ilifanya pasiwepo na migongano yoyote ya matumizi ya ardhi, pia hapakuwepo na maendeleo yoyote ya kisayansi na kiteknolojia sehemu za ardhi ziliweza kutengwa, kwa urahisi, kwa ajili ya kuhifadhi Wanyamapori bila kuwaathiri sana watu walioshi karibu na maeneo hayo.

Lakini Leo, idadi ya watu Tanzania imeongezeka na kufikia takribani watu milioni 62 na kuna maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia, vitu ambavyo hufanya ardhi iwe kidogo na kusababisha kuhitajika kwa mipango ardhi na sera ya wazi ya kuhifadhi wanyamapori

Wanyamapori wa Tanzania ni urithi wa asili wa pekee na raslimali yenye umuhimu mkubwa kitaifa na kimataifa.