Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Morogoro
Ofisi ya makamu wa Rais, Kitengo cha Mazingira wakishirikiana na Shirika la Uhifadhi Mazingira Duniani (WWF) ,wamekutana na wadau mbalimbali jijini Morogoro kujadili namna ya kuboresha rasimu ya mpango mkakati wa uhifadhi bionuai nchini.
Akizungumza na Jamhuri Digital,Ofisa Elimu Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Martha Ngalowera amesema wamekutana na ,wadau mbalimbali kwenye kikao kazi maalum cha kuboresha mpango mkakati wa utekelezaji wa Uhifadhi Bioanuai (NBSAP).
Matha amesema lengo kuu ni, kufanya kazi ya upitiaji rasimu ya uandaaji wa mpango mkakati wa ulinzi wa bioanuai ambao umeandaliwa na watalaamu waelekezi walioteuliwa na Serikali.
Amesema Serikali imewashirikisha wadau, ili waweze kuwa mpango mkakati utakaoiwezesha jamii kushiriki katika uhifadhi wa Bioanuai kwa sababu ndizo zinazoleta maendeleo ya nchi.
“Faida nyingine ya uhifadhi Bionuwai,tunaiona kwenye sekta ya kilimo na afya pale ambapo tunategemea misitu kwa chakula na dawa ikihalibiwa hatuwezi kupata huduma ‘’amesema.
Matha amesema mkutano utakuwa chachu kwa jamii,kwenye utunzaji Bioanuai kuwa endelevu.
Mmoja wa washiriki Rajabu Majidu kutoka Rufiji amesema kupitia mkakatii huo wa kimataifa, una vitu vingi ambavyo vinapangwa kutekelezwa katika ngazi ya chini hivyo jamii haina budi kuutambua vizuri.
“Utaleta manufaa kwa sababu wahifadhi wakuu ni wanajamii, ambao huko ndiko kwenye ukataji wa miti na wasababishi wa mabadiliko tabia nchi ni wazi wakielimishwa wataelewa umuhimu na watapunguza ukataji miti hovyo na wataweza kutunza Bainuwai
Mfano wavuvi wakielimishwa, wataweza kutunza viumbe wa bahari”amesema
Steven Kapinga kutoka Global Youth Biodiversity Network amesema , mkutano umejaribu kuangalia ni namna gani makubaliano yanaweza kuleta matokeo chanya kwa Wanawake, Vijana na Jamii kwa ujumla
Kapinga amesema kupitia malengo au shabaha za mpango mkakati ni kusimamia, Baionuwai nchini kuishi katika mazingira salama na endelevu.
Amesema wadau mbalimbali kutoka serikalini,asasi za kiraia na za kijamii ulikuwa na lengo la kuanzisha ,mjadala wa kupitia mpango mkakati wa kusimamia na kuhifadhi Bionuai kuelekea mkutano wa nchini wanachama mwezi ujao (NBSAP)
“Katika mambo tuliyo jadili ni pamoja na ushirikishwaji jumuishi, wakati wa utekelezaji na kuhakikisha Wizara zinasomana kwenye sera ili kurahisisha shughuli za usimamizi wa Bainuwai zina imarika ambapo kila mwananchi anapaswa kujua umuhimu wake na namna gani atashiriki katika suala zima la uhifadhi na usimamizi wa binuai ili tuwe na uhifadhi endelevu.
Ofisa Sera na Uchechemuzi Maureen Mboka kutoka Shirika la Uhifadhi wa Mazingira na Wanyamapoli (WWF) amasema wameandaa mkutano huo kwa kushirikiana na Ofisi ya makamu wa Rais kitengo cha mazingira na wadau mbalimbali kutoka asasi za kiraia na kijamii ili waweze kuboresha malengo mahususi ya mipango ya utekelezaji wa mpango wa uhifadhi chini ya (NBSAP)
“Mpango huu ni utekelezaji wa maridhiano, ambayo yalikubaliwa katika mkutano wa kimataifa 2022 nchini Canada.
Katika mkutano ule , kulikuwa na maridhiano ya mikakati ya ulinzi wa viumbe ambapo kila nchi ilipewa jukumu la kwenda kutengeneza mpango mkakati kulingana na mazingira yake
Kwa hiyo sisi kama WWF ni wadau wa maendeleo kwenye masuala ya uhifadhi tumefadhili mradi huu kwa kuwakusanya wadau kutoa maoni yao kwenye mpango mkakati wa ulinzi wa bionuwai unakamilika
lengo ni kufanya ushirikishwaji kwa jamii yote, ili kama kuna vitu ambavyo vinatakiwa viboreshwa kabla hatujakwenda kuwasilisha kimataifa Colombia mwezi ujao
Tunategemea uwepo wao wataweza kupeleka ujumbe kwa jamii ili waweke kwenye mipango yao.