Na Dotto Kwilasa,JamhuriMedia,Dodoma
WIZARA ya Elimu Sayansi na Teknolojia
nchini,iko mbioni kuzindua Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014, Toleo la 2023 na Mitaala Iliyoboreshwa Januari 31,2025 Jijini Dodoma.
Hatua hiyo ni kufuatia Serikali kusikia michango na hoja mbalimbali zinazotolewa na wadau kuhusu mfumo wa Sera ya Elimu hivyo inaendelea kufuatilia majibu ya hoja zote zinazotolewa ziwepo ndani ya Sera hiyo.
Aidha mabadiliko hayo yanalenga kuongeza tija kwenye mfumo wa elimu ambapo utekelezaji wa Mitaala hiyo utafanywa kwa awamu kulingana na mageuzi yaliyopo kwenye sera ya elimu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 10,2025 hapa Jijini Dodoma, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda amesema Sera ya Mitaala hiyo tayari imeshaidhinishwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia kikao cha Baraza la Mawaziri na kueleza kuwa ndiye atakayezindua Mitaala hiyo.
“Mitaala iliyoboreshwa ni maono juu ya mageuzi makubwa katika sekta ya Elimu,kwa kuzingatia umuhimu huo tayari sera ya mitaala imefanyiwa mapitio na kubadilishwa ili kuendana na sera ambayo tunayo,mabadiliko hayo yataenda kugusa vizazi na vizazi kwani ukamilifu wa utekelezaji wake ni kuanzia elimu ya awali mpaka kidato cha Sita, “amesisitiza.
Amesema licha ya kuwa mchakato wake utachukua muda kutokana na kuanza hatua kwa hatua, mabadiliko yake yataenda kuleta muelekeo ambao utabadilisha taswira ya elimu nchini.
“Mfano mjadala mkubwa unaoendelea kwasasa nchini ni kuhusu somo la Kingereza, ukienda kwenye sera utaona suala la lugha, ukienda kwenye mitaala utakuta ufundishaji wa lugha, tunasikia watu wanazungumza suala la akili mnemba ni suala kubwa sana lakini ukieda kwenye sera suala la tehama na mambo yote yanayohusiana na mambo haya yanayozungumzwa ukija kwenye mitaala utaona yanavyotekelezeka na kushughulikiwa,”amesema.
Pia mezungumzia suala la kufundisha ujuzi unaomuandaa mwanafunzi na dunia ya sasa na mabadiliko makubwa yanayotoka duniani kweda mbele sera hiyo inaelezea namna ya wanavyoshughulikiwa na mitaala inaeleza yanavyotekelezwa.
“Kufutia mabadiliko hayo tayari maandailizi ya kuwapiga msasa walimu yameshaanza na ajira kwa walimu 4000 wa somo la biashara tayari zipo kwenye mchakato