Wizara ya afya katika Ukanda wa Gaza inayodhibitiwa na kundi la Hamas imesema leo Jumamosi kwamba watu 921 wameuawa katika eneo la Palestina tangu Israel ilipoanzisha wimbi jipya la mashambulizi mnamo Machi 18 mwaka huu.

Wizara ya afya katika Ukanda wa Gaza inayodhibitiwa na kundi la Hamas imesema leo Jumamosi kwamba watu 921 nwameuawa katika eneo la Palestina tangu Israel ilipoanzisha wimbi jipya la mashambulizi mnamo Machi 18 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na wizara hiyo ni kwamba idadi hiyo inajumuisha watu 25 waliouawa katika muda wa saa 24 zilizopita. Taarifa hiyo imeeleza pia, idadi jumla ya waliouawa tangu kuanza kwa mzozo huo Oktoba 7 mwaka 2023 sasa imefikia watu 50,277.

Mazungumzo ya amani yamekwama baada yaIsrael na Hamas kushindwa kuafikiana hadi sasa kuhusu namna ya kuendeleza makubaliano ya usitishwaji mapigano huko Gaza.