Msemaji wa Shirika la Afya Ulimwenguni WHO Tarik Jasarevic amesema kufunga mipaka hakutazuia kusambaa kwa virusi vya homa ya nyani.
Ameiambia DW kwamba uzoefu unaonyesha kwamba kufunga mipaka hakutasaidia kuvizuia virusi, akiangazia hatua kama hiyo ilipochukuliwa wakati wa janga la UVIKO-19.
Na badala yake amesema kinachotakiwa kufanyika ni kuhakikisha waathirika wanatambuliwa ili wasiwaambukize wengine na kutoa wito wa upimaji wa mara kwa mara na watu kujichunguza ikiwa wana dalili za maambukizi ya mpox.
Ameyaomba pia mataifa kuimarisha mifumo ya kiafya katika kufuatilia maambukizi ya maradhi hayo.
Tutumie maoni yako.