Afisa wa ngazi ya juu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ameonesha wasiwasi juu ya uwezekano wa miripuko katika Gaza iliyokumbwa na vita baada ya virusi vya ugonjwa wa kupooza kugunduliwa kwenye maji taka

Ayadil Saparbekov, ambae ni mkuu wa huduma za dharura wa shirika hilo katika maeneo ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu, alisisitiza kuwa “bado hawaja kusanya sampuli za binadamu” kwa hivyo bado haijafahamika ikiwa kuna mtu yeyote aliyeambukizwa virusi hivyo.

“Nina wasiwasi sana kuhusu mripuko unaotokea Gaza. Na hii sio polio pekee – miripuko tofauti ya magonjwa ya kuambukiza ambayo inaweza kutokea huko Gaza. Kulikuwa na hepatitis A iliyothibitishwa mwaka jana na sasa tunaweza kuwa na polio.

Lakini juma lililopita mashirika ya Umoja wa Mataifa yalisema Mtandao wa Maabara wa Kimataifa ya Polio ulipata virusi vya polio aina ya pili vilivyotokana na chanjo katika sampuli sita za kimazingira zilizokusanywa kutoka kwa maji taka katika Ukanda wa Gaza mwezi Juni 23.

Please follow and like us:
Pin Share