Mtendaji mkuu wa zamani wa Manchester United ya England, David Gill ameangalia uwezo wa timu hiyo kwa sasa akatikisa kichwa kisha akasema, “Hawa sio mashetani wekundu ninaowajua.”
Bila kutafuna maneno wala kupepesa macho na kutikisa masikio, Gill amesema, “Ninachokiona kwa sasa kwa Kocha Louis van Gaal ni kama amechemsha msimu huu.”
Ikicheza nyumbani, Jumamosi iliyopita United ilipigwa 1-0 na Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu England hivyo kuwashusha mashetani hao wekundu kutoka nafasi ya tano hadi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu England. Tottenham ikachukua nafasi yake.
Baadhi ya mashabiki wa timu hiyo ya Old Trafford waliizomea timu hiyo baada ya filimbi ya mwisho wakionesha kusononeka kwa matokeo ya kufungwa 1-0 na Southampton.
“Wote tulijua kwamba angalau kwenye mchezo ule (Jumamosi iliyopita) matokeo yangekuwa mazuri, lakini wapi bwana, tumepigwa,” alisema Gill ambaye ni mmoja wa wakurugenzi wa klabu hiyo alipofanya mahojiano na BBC Radio 5.
“Najua kila mmoja namna anavyopata taabu kwa jinsi timu inavyochemsha. Kwa hali hii nashauri jambo moja tu, hatuna sababu ya kuparaganyika. Tuwe pamoja,” alisema kwa huzuni.
Gill amesema asingependa kuzungumzia hatima ya Kocha Van Gaal katika klabu hiyo akidai uamuzi pekee utafanywa na wamiliki wa timu akina Glazers pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Ed Woodward.
Wachambuzi wa soka wanasema kitu kimoja ambacho Kocha Van Gaal mwenye umri wa miaka 64 anashindwa kuelewa ni namna ya kupangilia staili ya kucheza kwa timu hiyo huku akielezwa ana kikosi bora.
Inaelezwa kwamba United iliweza kulifikia lango la Southampton mara moja tu ambako sasa imecheza zaidi ya saa 8 na 26 bila ya kufunga bao kipindi cha kwanza.
“Nitakuwa mnafiki nikisema kwamba eti timu inafanya vema,” aliongeza Gill, ambaye kabla ya filimbi ya mwisho aliamua kubadili burudani na kwenda Jumba la Sinema badala ya kuiangalia Manchester United.
“Kwa maoni yangu, United ya enzi zetu ilikuwa bora na tuliwaagiza wachezaji cha kufanya. Lakini naona sasa inarudi ileile ya miaka 1950 inayocheza kwa mkondo mmoja. Tunataka timu ikabe na hapo ndipo tunaweza kusonga mbele.”
Manchester United imeshinda mataji 20 ya Ligi Kuu England 13 kati yake ni ya Ligi Kuu, wakati timu hiyo ikinolewa na Babu Sir Alex Ferguson.
Van Gaal ana kazi kubwa kuikuta Leicester ambayo kwa sasa inaongoza ligi hiyo kabla ya mchezo wa Jumapili kati ya Arsenal na Chelsea.
“Ushindi gani wa kubahatisha,” anasema Gill na kuongeza: “Tunamkumbuka sasa Sir Alex Ferguson na kuamini kwamba kumbe alikuwa anafanya kazi ya ziada.
Shabiki mmoja wa United ametuma barua nzito United akitaka Van Gaal akae benchi na nafasi yake aikamate Ryan Giggs, ambaye kwa sasa ni msaidizi wa kocha huyo wa Kidachi.
Gigs ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 42, ni nyota wa zamani wa kimataifa wa
Wales ambako amekuwa Manchester United, kama mchezaji wa muda mrefu alikovuna mafanikio mengi na sasa yuko kwenye benchi la ufundi. Yuko United yangu mwaka 1990.
Debe kwa Giggs limepingwa na Gill hinted that Giggs akisema Ryan bado ni mchanga kupambana na changamoto za United, lakini wamiliki wakimtaka ni vema wakajiridhisha.
Taarifa kwamba tayari Jose Mourinho, eti amendika barua kuomba kibarua cha kumrithi Van Gaal zimepingwa na wakala wa kocha huyo mreno, akisema habari hiyo inachekesha.
Kuna taarifa zinasema kwamba Mourinho ameandika barua yenye kurasa sita kutaka kuinoa United na wakala wake ameibuka ghafla akisema, “si za kweli”, amenukuliwa Mendes akiikana barua hiyo kwa nguvu zote.
Gazeti la The Independent la Jumapili iliyopita, liliripoti madai kuwa Mourinho ameandika barua hiyo ya kuonesha mahaba yake na Manchester akielezea mikakati yake ya kufumua na kuisuka upya United.
Mourinho mwenye umri wa miaka 52, kwa sasa anapatikana baada ya kutimuliwa Chelsea Desemba, mwaka huu.
“Wanaweza kunitimua wakitaka. Hilo sikatai hata kidogo na zaidi ya hapo nimeona tulivyocheza,” anasema kocha huyo mwenye umri wa miaka 64.