Na Isri Mohamed, JammhuriMedia, Dar es Salaam

Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Ezekia Wenje ameonesha kusikitishwa na kauli zilizotolewa na Godbless Lema akimtaka Lissu kumteua Dkt Silaa kuwa mjumbe wa kamati kuu wa Chadema, mara tu atakaposhinda nafasi ya uenyekiti anayoigombea.

“Dkt Silaa ni kada wa CCM, unaposikia leo Lema anamshauri Lissu kwamba akishinda uenyekiti amteue kada wa CCM kuwa mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA hii ni kitu ‘serios’ sana”

“Sasa huyu Silaa wanayemsema aliandika kitabu cha ‘Nyuma ya pazia’ kinachoiita CHADEMA kuwa ni chama cha magaidi, sheria za vyama vya siasa haziruhusu chama cha siasa kuwa cha kigaidi, kwa hiyo Dkt Silaa alitaka chama chetu kifutwe”