Waziri wa biashara wa New Zealand Andrew Bayly amejiuzulu kama waziri wa serikali baada ya ‘kuigusa’ sehemu ya juu ya mkono wa mfanyakazi wake wiki iliyopita, katika kile alichoelezea kama tabia ya ‘kupindukia’.

Bayly alisema siku ya Jumatatu kwamba “anasikitika sana” kuhusu tukio hilo, ambalo alilielezea kuwa sio hoja bali “majadiliano ya kusisimua”.

Kujiuzulu kwake kumekuja baada ya kukosolewa mwezi Oktoba mwaka jana kwa kumuita mfanyakazi wa kiwanda cha mvinyo “mpotevu”- ikiwa ni pamoja na kuweka vidole vyake katika umbo la ‘L’ kwenye paji la uso wake – na kudaiwa kutumia lugha ya dharau dhidi yake. Baadaye aliomba msamaha kwa umma.

“Kama wengi wenu mnavyojua, nimekuwa na papara kuendesha mabadiliko katika nyadhifa zangu za uwaziri,” Bayly alisema katika taarifa yake kutangaza kujiuzulu.