WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga katika akiwa na baadhi ya viongozi wa timu ya Coastal Union wakati akipokwenda kuwakabidhi kiwanja eneo la Maweni Jijini Tanga kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya City Plan Consultants (T) Limited Dkt Juma Mohamed |
Waziri wa Afya maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa halfa ya makabidhiano hayo yaliyofanyika Mtaa wa Kichangani Kata ya Maweni Jijini Tanga
Diwani wa Kata ya Maweni(CCM) Colvas Joseph akizungumza katika hafla hiyo
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa timu ya Coastal Union akizungumza katika halfa hiyo. |
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoani Tanga (TRFA) Saidi Soud kushoto akiteta jambo na Waziri wa Afya maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga
Mwenyekiti wa baraza la wazee timu ya Coastal Union Salimu Bawaziri akizungumza
Waziri wa Afya maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu kushoto akiteta jambo na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji katika halfa hiyo kushoto ni Mwenyekiti wa TRFA Saidi Soud na Mwenyekiti wa timu ya Coastal Union Steven Mguto
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akimsikiliza kwa umakini Diwani wa Kata ya Maweni (CCM) Colvas Joseph
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akishiriki kucheza wakati wa halfa hiy |
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameipongeza Kampuni ya City Plan kwa kuunga mkono juhudi zao za kutaka kuimarisha klabu ya Coastal Union “Wagosi wa Kaya” kwa kuisaidia kupata kiwanja chao eneo la Maweni Jijini Tanga.
Hatua hiyo inatokana na viongozi kufanya kazi kubwa wakishirikiana na wadau kuhakikisha wanapambana ili kuiwezesha timu hiyo kurudi kucheza michuano ya Ligi kuu Tanzania Bara msimu ujao baada ya kucheza madaraja ya chini kwa kipindi.
Kiwanja hicho ambacho kina ukubwa wa square mita 7632 kipo Mtaa wa Kichangani Kata ya Maweni ambacho kina gharimu kiasi cha sh.milioni 38 kimepatikana baada ya kuwepo kwa juhudi kubwa za Waziri Ummy kuiomba kampuni hiyo kuisaidia timu hiyo eneo lake la kiwanja.
Kukabidhiwa kwa kiwanja hicho inafungua ukurasa mwengine wa mafanikio kwa timu hiyo kongwe hapa nchini.Akizungumza leo wakati wa hafla ya makabidhiano ya kiwanja hicho, Waziri Ummy alisema kitendo cha kampuni hiyo kutoa eneo hilo kimesaidia mipango iliyokuwa nayo timu hiyo kuanza kwenda vema huku wakijipanga kwa hatua nyengine.
Alisema suala hilo linatokana na mshikamano uliopo baina ya viongozi waliopo wakiwemo wapenzi, mashabiki na wanachama huku wakiwataka kuuendeleza ili kuweza kupata mafanikio makubwa siku zijazo kwenye michuano ya ligi kuu.
“Kwanza niwapongeze timu ya Coastal Union kwa kuonyesha mshikamano na kuweza kupanda daraja kucheza ligi kuu na kama mtu anafanya vizuri watu wengi wanakuwa tayari kuweza kuwaunga mkono “Alisema.
Alisisitiza kuwa kufanya vizuri kwa timu hiyo kumefanya kuvuta wadau ambao wameweza kuwasaidia kiwanja nawashukuru kwani wakati tunapongezana nilihaidi kuwatafutia wadau pia niwaambie bado tunaendelea kutafuta wadau na nihaidi hata ile block yenye square mita 9600 yenye thamani milioni 48 atatafuta wadau ili waweze kupata eneo hilo.
Alisema atasaidia kutafuta wadau ili kupata eneo hilo ambalo litakuwa kwa ajili ya matumizi ya ujenzi wa Hosteli,Gym na Ukumbi wa sherehe wa Coastal Union kwa sababu watu wa Tanga wana fanya sherehe na kitchen party kila siku .
Hata hivyo alisema pia katika kiwanja ambacho wamekabidhiwa timu hiyo leo atagharamia gharama za hati za usajili mpaka kupata hati yenye jina la klabu ya Coastal Union na baadae atakwenda kuwakabidhi
Waziri huyo alitoa wito kwa wakazi wa Jiji la Tanga wanaotaka kuwekeza waende eneo la Pongwe ambalo lina viwanja 937 hivyo watu waende kuwekeza kwa sababu Coastal Union wakiwa hapo itavutia lakini pia ameitaka kampuni hiyo kuwepo kwa eneo kwa ajili ya zahanati kama walivyofanya kutoa kwa shule ya Msingi.
Naye Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Mayeji alimpongeza Waziri Ummy kwa kazi kubwa kwa kuongea na wadau kuona Coastal Union inapata sehemu ya kufanyia mazoezi na mafunzo ya soka kwani jambo hilo linaonyesha namna alivyokuwa na dhamira kubwa ya kusaidia kuinua michezo mkoani Tanga akiwa namba moja Sports Lady namba moja.
Kwa hilo Mh Waziri umefanya kazi kubwa sana kwani hatua hiyo inaisongeza timu ya Coastal Union kwenye mafanikio kutokana na kupata eneo ambalo wataweza kulitumia kufanya mazoezi na masuala mengine ya kimichezo “Alisema
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Coastal Union Steven Mguto alisema furaha kubwa aliyonayo huku akiimshukuru Waziri Ummy kwa kuisaidia timu hiyo kwa hatua yake ya kuisaidia timu hiyo kuweza kurudisha heshima yaa soka mkoa wa Tanga
“Mh Waziri hapa nilipo nimeishiwa maneno ila nisema mama Ummy umetusaidia sana ulikuwa wapi siku zote kauli ya Mungu anasema nitakuwa muda na saa usizotarajia kila tunapofanyaa tukio kubwaa tunaona nyota inatuandama tulipata basi wakati tunapanda daraja kipindi kile safari hii tumepanda nyota nyengine imekuja kiwanja tuendelee kuomba na kushikamana”alisema.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Tanga (TRFA) Saidi Soud alisema tumehemewa na furaha kwenye jambo hilo ambalo ni la kihistoria kutokana na Waziri Ummy kuwa mama wa kweli kwa kuwashika mkono.
“Labda nisema Waziri Ummy ni mama wa kweli nakumbuka wakati unasema utatushika mkono huko mbele tulikuwa tunasuasua lakini ujio wako umesaidia kuvunja hata makundi yaliyokuwa yakirudisha nyuma maendeleo “Alisema
Akizungumza katika Halfa hiyop, Mkurugenzi wa Kampuni ya City Plan Consultants (T) Limited Dkt Juma Mohamed alisema walipata ombi kutoka kwa Waziri Ummy Mwalimu kuona namna ya kupata eneo la Michezo kwa timu ya Coastal Union
Alisema baada ya hilo waliweza kulijadili na kuliwasilisha kwa wadau ambao ni wananchi wa eneo la hapa na kuweza kupatikana kwa eneo hilo ambapo pia walitoa viwanja cha mpira ni hamsini kwa mia moja lakini panazaidi ya eneo la pitch ya mpira.
Tulikubaliana kuhifadhi viwanja 16 upande block za chini kuna masuala wanaendelea na majadiliano vitalipiwa kwa ajili ya kuweka maeneo mbalimbali ya michezo.
Naye Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku alisema mambo hayo yote yanatokea kwa sababu watu wapo pamoja hiyo kuwataka kuendelea kushikamana kwa kumuomba mwenyezi mungu siku zijazo ili waweze kupata mafanikio zaidi.
Hata hivyo alisema uongozi ni uongozi huku akiwataka viongozi wasiogope kurushiwa maneno badala yake washirikiane kuhakikisha klabu hiyo inafanana na hadhi yake iliyokuwa nayo ya miaka ya nyuma.
Awali akizungumza Mkuu wa wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa alisema jambo ambalo limefanywa na Waziri Ummy ni nzuri na la kupongeza kwani msaada wake ndani ya timu hiyo ni mkubwa sana.
Alisema atajitahidi kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella ili kuwasaidia kwa ajili ya kupata mafanikio makubwa zaidi
“Lakini nimpongeza Mh Waziri kwa kutusaidia kufanikisha na kurudisha umoja na ushindi kwenye timu hiii, tuache na tusahau yaliyopita tugange yajayo “Alisema