Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Shirikisho la Urusi nchini, Andrey Avetisyan katika ofisi za Wizara Jijini Dodoma leo Mei 31, 2023.

Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamekubaliana kuimarisha ushirikiano wa kihistoria na kidiplomasia uliopo baina ya Tanzania na Urusi pamoja na sekta za ushirikiano zilizo katika hatua mbalimbali kwa maslahi ya pande zote mbili.

Vilevile, katika mazungumzo hayo wamejadili juu ya mkutano wa Urusi – Afrika na Kongamano la Uchumi litakalofanyika mwezi Julai 2023 nchini Urusi. Kongamano hilo linatarajiwa kutoa mtazamo wa uhusiano kati ya Urusi na na nchi za Afrika.

Tanzania na Urusi zinashirikiana katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ulinzi, afya, biashara, viwanda, uwekezaji na utalii ambapo kwa pamoja zimekubaliana kuendeleza ushirikiano huo ili kuleta tija katika utekelezaji wa diplomasia ya uchumi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisalimiana Balozi wa Shirikisho la Urusi nchini, Andrey Avetisyan baada ya kuwasili katika ofisi za Wizara jijini Dodoma kwa mazungumzo
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax (kulia) katika picha ya pamoja na Balozi wa Shirikisho la Urusi nchini, Andrey Avetisyan baada ya kuwasili katika ofisi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Dkt. Stergomena Tax (kulia) katika picha ya pamoja na Balozi wa Shirikisho la Urusi nchini, Andrey Avetisyan baada ya kuwasili katika ofisi