Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) tarehe 15 Oktoba, 2024 amejiandikisha katika Daftari la Mkazi katika kituo kilichopo Kitongoji cha Unyamwezini Kata ya Itumbili Wilayani Magu.

Mara baada ya kuwasili katika Kituo cha kuandikisha wapiga kura,Waziri Tax alilakiwa na Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe. Joshua Nasari na Afisa Uchaguzi wa Wilaya ya Magu Bw. Mwagala Charles Masunga na
baada ya kujiandikisha, Waziri Stergomena akatumia wasaa huo kumpongeza Mkuu wa Wilaya ya Magu Joshua Nasari kwa kazi nzuri anayoifanya katika uandikishaji huu wa daftari la makazi la wapiga kura katika Serikali za mitaa kwenye Wilaya ya Magu.

Pia Mhe. Waziri akasema kuwa taarifa aliyopewa na Afisa Uchaguzi wa Wilaya ya Magu Bw. Mwagala Masunga inatia moyo sana, kuongeza “kama tunavyofahamu wote Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alifungua zoezi hili kuonesha umuhimu wake tarehe 11 Oktoba, 2024 ambayo ndiyo siku alijiandikisha huko Dodoma ambako ndiyo makazi yake, na ndiyo maana na mimi nimekuja Wilayani Magu kujiandikisha ambapo ndiyo makazi yangu.

Aidha, Waziri Dkt. Stergomena akasisitiza kuwa amefurahi sana kupata fursa ya kujiandikisha pia akatoa wito kwa Wana Magu wenzake na wananchi wote nchini kwenda kujiandikisha kwani hili ni zoezi muhimu sana nchini na akasisitiza kuwa uongozi unaanzia kwenye maeneo yetu tunayoishi tusipojiandikisha katika daftari la kupiga kura la mkazi tutakosa fursa ya kuchagua viongozi watakaokuletea maendeleo.

Amesema Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mambo mengi kama mlivyojionea wakati Mwenge wa Uhuru tulivyoupokea hapa Magu ukizindua miradi mbalimbali ya maendeleo miradi hiyo imetokana na Uongozi bora wa Mheshimiwa Rais Samia ambaye ameonyesha njia lakini huku kwetu chini kuna DC na Mkurugenzi wa Halmashauri ambao hawawezi kufanya kazi peke yao lazima tuchague viongozi makini watakaosaidiana nao kutuletea maendeleo.

.   

Please follow and like us:
Pin Share