Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dodoma

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa (Mb), ameiagiza Bodi mpya ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kuhakikisha inasimamia kwa ukaribu utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano vijijini.

Akizungumza katika uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika leo tarehe 4 Februari, 2025 kwenye Makao Makuu ya Ofisi za UCSAF jijini Dodoma, Silaa amesema, mradi wa ujenzi wa minara hiyo ni sehemu muhimu ya mkakati wa Serikali wa kuleta mageuzi ya Kidijitali katika maeneo ya vijijini, ambapo zaidi ya wananchi milioni 8.5 waishio vijijini watafikiwa na mawasiliano pindi mradi huo utakapokamilika.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa (Mb), akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) uliofanyika leo tarehe 4 Februari, 2025 jijini Dodoma.

“Mradi huu ni wa kimkakati, nawaagiza Bodi kuhakikisha mnawasimamia watoa huduma na kuwaagiza wawasilishe mipango kazi yao inayoonesha kuwa ifikapo Mei 12, 2025 watakuwa wamekamilisha ujenzi wa minara yote” alisisitiza Waziri Silaa.

Aidha Waziri huyo ameitaka bodi kuzingatia miongozo, taratibu na sheria za uendeshaji wa shughuli za Bodi, ili kuhakikisha utekelezaji wa majukumu yao unakuwa wa ufanisi na wenye tija.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohammed Khamis Abdulla amesema, UCSAF imepewa jukumu la kufikisha huduma za mawasiliano katika maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara, ambapo tangu kuanzishwa kwake imefikisha huduma hiyo muhimu katika kata 1,582 zenye vijiji 4,396, kwa kujenga jumla ya minara 1,725 ambayo inatoa huduma kwa wananchi milioni 23.9.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Mohammed K. Abdulla akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi mpya ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) iliyofanyika leo tarehe 4 Februari, 2025 jijini Dodoma.

Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya UCSAF, Mhe. Balozi Valentino Mlowola, ameahidi kuwa bodi yake itaendelea kushirikiana na wadau wa sekta ya mawasiliano ili kuleta maendeleo endelevu katika sekta hii muhimu.
Ameongeza, bodi pia itajitahidi kuleta ufanisi kwa kutumia rasilimali zilizopo ili kuhakikisha ufanisi wa miradi yote inayotekelezwa na UCSAF

UCSAF ilianzishwa na Serikali ya Tanzania kwa Sheria ya Bunge Sura ya 422 mwaka 2009, na ilianza kazi rasmi Julai 1, 2009. Malengo ya kuanzishwa kwake ikiwa ni kufikisha huduma za mawasiliano katika maeneo ya vijijini, ambayo hayana mvuto wa kibiashara na ambayo ni vigumu kwa watoa huduma za simu kufikisha huduma za mawasiliano.

Mwenyekiti wa Bodi ya UCSAF, Mhe. Balozi Valentino L. Mlowola, akitoa neno la shukrani wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanyika leo tarehe 4 Februari, 2025 jijini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wapya wa Bodi ya UCSAF wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanyika leo tarehe 4 Februari, 2025 jij