Na Cresensia Kapinga, Jamuhuri, Songea.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Damas Ndumbaro amewataka Watanzania kutunza na kuendeleza urithi wa tamaduni zetu ambapo amewataka wazazi kukemea mmomonyoko wa maadili kwenye jamii na kufuata mila na desturi za kitanzania
Agizo hilo amelitoa Septemba 20,2024 wakati akizinduaTamasha la tatu la Kitaifa la Utamaduni lililofanyika kwenye viwanja vya Maji Maji,Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma,amesema, wasitumie haki za binadamu katika kukiuka miiko na kuharibu mila na desturi za nchi yetu, lazima wafundishe mila na desturi za kitanzania na historia yetu kwa Watoto kwani ni taifa la kesho.
Alisema,”Watanzania tunapaswa kudumisha upendo, ushirikiano, utulivu na amani ambapo kupitia tamasha hilo wataweza kuelewa umuhimu wa amani na kufata mila na desturi zetu ili kuondokana na utandawazi ambao hauna maana .Tuwafundishe Watoto wetu maadili mema, mila na desturi zetu na hata historia kwa kufata kauli mbiu yetu ya “Utamaduni wetu ni utu wetu tuenzi na kuuendeleza “alisema Waziri Ndumbaro.
‘’ Familia zimekuwa mstari wa mbele kulalamikia mmomonyoko wa maadili badala ya kutoa elimu kwa watoto wetu, taasisi za dini , watu maarufu na vyombo vya habari zikiwemo shule kuanzia ngazi ya chekechea hadi vyuo vikuu vitusaidie kupambana na mmomomyoko wa maadili “alisema Dkt.Ndumbaro.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas amesema Mkoa wa Ruvuma unatambua umuhimu wa utamaduni na ndio maana hawakusita kuwa wenyeji wa Tamasha hilo la tatu la kitaifa la utamaduni .tunatambua umuhimu wa kukuza sanaa na michezo kwenye taifa hili.
Amesema, Tamasha hilo ni fursa ya kukuza ichumi wa Mkoa wa Ruvuma hivyo amewakaribisha wageni wote toka ndani na nje ya mkoa kutembelea vivutio vilivyopo kwenye mkoa wa Ruvuma .
“Nimefarijika kuona bado Mkoa wa Ruvuma tunaongoza kwa hivyo karibuni kwenye tamasha letu hili kubwa la kitaifa na mwendelee na shamra shamra kama kawaida kwani ,mkoa upo salama hivyo tunawakaribisha wananchi wote waje kushiriki,”alisema Abbas.
Naye Naibu Waziri Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Hamisi Mwinjuma amesema , tamasha hilo ni muhimu kwani litasaidia wananchi kukumbushwa mila na desturi za Mtanzania , hivyo itasaidia kuondoa ushoga na usagaji na litaendelezwa.
Alisema ,Tamasha la Utamaduni la Kitaifa linaendelea kukua mwaka hadi mwaka hivyo wataendelea kusimamia maelekezo ambayo yametolewa na Rais Samia asukuhu Hassan ili kuwasaidia wananchi kufata mila na desturi za kitanzania.
“ Tamasha hili lina faida nyingi zinakuja kupitia tamasha hilo kwani watu wengi wanaenda mkoa wa Ruvuma , ambapo mh. Rais alitoa maelekezo kuwa Tamasha hili la utamaduni lifanyike kila mwaka kwenye mikoa tofauti tofauti ili wananchi wapate nafasi ya kujua utamaduni mbali mbali ya makabila yao