Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amewataka Wanachama wa Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA), kutumia vizuri majukwaa yao ya habari mtandaoni kujipatia kipato ili kukuza maisha yao.

Waziri Nape ameyasema hayo alipokutana na wadau wa jumuiya hiyo leo Julai 5, 2024 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam ili kujadili mambo mbalimbali ya kuboresha tasnia ya habari mtandaoni.

“Tunafuatiliwa na watu wengi mtandaoni na wengi wanatuamini, wanatuelewa, ninachotaka kuwaomba ni kwamba ni vizuri tutumie mitandao hiyo vizuri kwa sababu tuna nchi ambayo tuna wajibu wa kuilinda na kuendelea kuwa katika utulivu, wajibu huo ni wetu sote”, amesema Waziri Nape.

Aidha, Waziri Nape amewahimiza wanachama wa jumuiya hiyo ya wanahabari kutimiza wajibu wa kufichua maovu huku wakitimiza wajibu wa kuilinda nchi.

Awataka pia wanahabari kujikita katika utaalam wa maeneo mbalimbali (Professionalism) ili kuandika habari katika maeneo hayo mahususi.

Please follow and like us:
Pin Share