Na Magrethy Katengu, JamhuriMedia, Dar es salaam
WAZIRI MKUU Mstaafu Kayanza Mizengo Pinda amewataka Vijana kutumia fursa ya Mageuzi ya Elimu Nchini kwa kujiunga vyuo stahiki vya Veta vinavyotoa Elimu ya ujuzi na Ufundi stadi ili kuwasaidia kuendesha Maisha yao na kuinuka kiuchumi
Kauli hiyo ameutoa leo Machi 20 ,2025 alipohudhuria mjadala wa wadau wa Veta Ikiwa ni siku ya tatu ya maadhimisho ya miaka 30 ya VETA yanayofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

“Hakika tulipotoka ni mbali miaka 30 iliyopita hatukuweza kutengeza kazi nzuri na za kibunifu tulikuwa tukiziona katika mataifa yaliyoendelea lakini hatimaye sasa kila kitu kizuri na chakiufanisi hupatikana hapa nchini hongereni Veta kwa kuwapika Vijana vizuri ” amesema.
Pamoja na pongezi hizo pia , Pinda ametembelea mabanda ya VETA nakujionea kazi mbalimbali za kibunifu na kivumbizi nakusema kwamba hakika Veta imenoa vijana inaendelea kutoa vijana mahili katika Nyanja mbalimbali za ufundi stadi.
“Ni ukweli usiopingika kwamba VETA imetoa mchango mkubwa sana katika taifa hili na mchango wake haupaswi kubezwa bali unapaswa kuimarishwa zaidi kwakuwa hakuna namna yoyote utakwepa ufundi stadi katika maisha yako kama binadamu” amesema Pinda.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha VETA , CPA Anthony Kasore amesema matunda ya veta yanayoonekana leo hii yamechangiwa kwa namna moja ama nyingine na Mheshimiwa Pinda wakati wa uongozi wake na hivyo huwezi kusema mafanikio ya Veta pasipo kumtaja mzee Pinda.
“Mzee wetu huyu alisimamia ipasavyo matunda ya VETA na leo hii amejionea mwenyewe namna ambavyo Veta ilivyo imarika, alikuwa akitushauri mambo kadha wa kadha ili kuhakikisha chuo kinafanikiwa katika utoaji wa huduma zake kwa jamii na taifa” amesema Kasore.
Maadhimisho hayo yanafikia kilele kesho na yatahitimishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu hasani na yalianza 18, Februari na yalizinduliwa na Waziri mkuu Kassim Kassim Majaliwa.
Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA) Iimepiga hatua kubwa kwakutoa wahitimu bora na wanaokubalika katika soko la ajira nchini ndani na nje ya nchi.


