Waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano Kassim Majaliwa amewataka wakulima wa zao la korosho Kuhakikisha wanapunguza na kuondoa Miti ya Mikorosho ambayo Inamiaka mingi shambani ambayo Inasababisha Kutoa mavuno hafifu na Yenye Ubora usiohitajika katika soko lakimataifa.
Majaliwa ameyasema hayo katika uzinduzi wa wa kampeni ya kitaifa ya upandaji wa Mikorosho Bora na Mipya Million10 katika Wilaya ya Ruangwa Mkoani lindi na Miche Hiyo imeandaliwa na Bodi ya Korosho CBT kwa lengo kuwaga kwa wakulima wa mikoa Inayolima zao la Korosho nchi Nzima ambayo inaanza Uzalishaji wa korosho Ndani ya kipindi cha Miaka3.
Waziri Mkuu anasema Wakulima wa zao la Korosho wanapaswa kubadilika kwa kupanda miche Mipya ilikuweza kupata Mavuno yenye Kuleta mafanikio.
Upandaji wa Mikorosho hiyo Unaanza Katika Msimu wa mwaka 2017/2018 ambapo matarajio ya miaka 5 mkapa 10 Ongezeko la uzalishaji utafikia Tani Laki7 kutoka Tani laki mbili na 65 za msimu wa mwaka jana.