Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akishiriki ufunguzi wa mkutano wa 19 wa Wakuu wa Nchi na Serikali Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM), katika ukumbi wa Ruwenzori, Kampala nchini Uganda, Januari 19, 2024. Waziri Mkuu amemuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Nchi na Serikali wakati aliposhiriki ufunguzi wa mkutano wa 19 wa Wakuu wa Nchi na Serikali Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM), katika ukumbi wa Ruwenzori, Kampala nchini Uganda, Januari 19, 2024. Waziri Mkuu amemuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo.
Rais wa Jamhuri ya Cuba Miguel Mario Diaz-Canel Bermudez akimkabidhi rasmi Rais wa Uganda Yoweri Museveni uenyekiti wa kundi la Umoja wa Nchi na Serikali 120 zenye Msimamo wa Sera ya Kutofungamana na Upande Wowote (NAM) katika ukumbi wa Ruwenzori, Kampala nchini Uganda, Januari 19, 2024. Mheshimiwa Majaliwa amehudhuria mkutano huo kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
Rais wa Uganda Yoweri Museveni, akizungumza baada ya kukabidhiwa uenyekiti, Mheshimiwa Museveni aliahidi kuwa chini ya uenyekiti wake atatoa ushirikiano wa kutosha kwa umoja huo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Januari Makamba akifuatilia ufunguzi wa mkutano wa 19 wa Wakuu wa Nchi na Serikali Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM), katika ukumbi wa Ruwenzori, Kampala nchini Uganda, Januari 19, 2024. Mheshimiwa Majaliwa amehudhuria mkutano huo kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye umoja wa Mataifa Balozi Hussein Kattanga akifuatilia ufunguzi wa mkutano wa 19 wa Wakuu wa Nchi na Serikali Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM), katika ukumbi wa Ruwenzori, Kampala nchini Uganda, Januari 19, 2024. Mheshimiwa Majaliwa amehudhuria mkutano huo kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)