Baadhi ya washiriki wa Ufunguzi wa Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Nchini wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza kabla ya kufungua Ofisi hiyo eneo la Mlimwa mjini Dodoma, Desemba 7, 2017
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akizungumza katika ufunguzi wa Ofisi yake uliofanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Dr. Augustine Mahiga kabla ya kufungua Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, eneo la Mlimwa mjini Dodoma, Desemba 7, 2017. Kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Alvaro Rodriguez.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Msanii maarufu wa mjini Dodoma Mwinamila baada ya onyesho la ngoma la kikunid cha msanii huyo kabla ya kufungua Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (kushoto kwake), eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mahariki, Dr. Augustine Mahiga akizungumza katika ufunguzi wa Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi w UNDP Nchini uliofanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kabla ya kufungua Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini eneo la Mlimwa mjini Dodoma, Desemba 7, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kabla ya kufungua Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini eneo la Mlimwa mjini Dodoma, Desemba 7, 2017. Wapili kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dr. Augustinew Mahiga na kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa Nchini, Bw. Alvaro Rodriguez
Waziri Mkuu,. Kassim Majaliwa akifungua Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017. Kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Bw. Alvaro Rodriguez.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP. nchini, eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017. Wapili kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez na wanne kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dr. Augustine Mahiga
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia baada ya kufungua Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017. Wapili kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez na wanne kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dr. Augustine Mahiga
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia ngoma ya msanii maarufu wa Dodoma, Mwinamila baada ya kufungua Ofisi ya Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017. Kushoto kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Dr. Augustine Mahiga na wapili kushoto kwake ni Mratibu Mkazi wa Mshirika ya Umoja wa mataifa ma Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Dodoma baada ya kufungua Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini , eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017. Watatu kushoto waliokaa ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mshariki, Balozi Dr. Augustine Mahiga na watatu kulia waliokaa ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Matifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Bw. Alvaro Rodriguez
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mwananchi baada ya kufungua Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata keki ikiwa ni moja ya shughuli za ufunguzi wa ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (kulia) eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mahariki, Dr. Augustine Mahiga.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua ofisi ya Umoja wa Mataifa na kusema uamuzi huo ni hatua muhimu ya kuendeleza mchakato wa Serikali wa kuhamia Dodoma.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Alhamsi, Desemba 7, 2017) wakati akizungumza na viongozi na watumishi wa taasisi za Umoja wa Mataifa waliohudhuria hafla ya ufunguzi rasmi wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa Dodoma, katika eneo la Mlimwa, Manispaa ya Dodoma.
“Wote mtakubaliana nami kwamba uzinduzi wa ofisi hii ya Umoja wa Mataifa ni hatua muhimu sana ya kuendeleza mchakato wa Serikali wa kuhamia Dodoma. Pia, inafungua mlango mpya utakaowezesha ofisi zote za kibalozi na mashirika ya kimataifa kujenga ofisi zao hapa Dodoma na kuhamia mapema,” alisema.
Alisema anatambua kwamba kwamba wapo viongozi na watendaji wenye hofu ya kuhamia na kuanza maisha mapya Dodoma. “Baadhi ya watendaji wanaogopa changamoto za kuhamisha watoto wao na wenza wao ili kuanza maisha mapya. Napenda kuwatoa hofu kwamba Dodoma ni mahali pazuri pa kuishi na kuna fursa nyingi,” alisema.
Alisema Serikali inaendelea kuboresha miundombinu iliyopo ya huduma za jamii na miundombinu ya barabara, maji, umeme na mawasiliano ili iwe bora zaidi. Alitumia fursa hiyo kuwasihi waombe maeneo ya ujenzi kwa ajili ya ofisi na makazi.
Aliushukuru Umoja wa Mataifa kwa kuiteua Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazotekeleza mfumo mpya wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa kuungana na kutekeleza shughuli zake kwa pamoja kama familia moja ya Umoja wa Mataifa yaani “UN Delivering as One”.
Naye Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dk. Augustine Mahiga alisema Umoja wa Mataifa unayo mashirika 50 na kwamba mashirika 23 kati ya hayo, yanafanya kazi zake hapa nchini.
Alisema wizara yake kwa kushirikiana na Manispaa ya Dodoma, watahakikisha kuwa mashirika hayo yanapatiwa viwanja vya kutosha ili kujenga ofisi zao mapema iwezekanavyo.
Mapema, Mwakilishi Mkazi wa UNDP na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania; Bw. Alvaro Rodriguez alisema wamefurahi kupata fursa ya kuwa taasisi ya kwanza ya kimataifa kuwa na Ofisi yake kwenye makao makuu ya nchi hapa Dodoma
“Tumefurahi kujumuika kwa pamoja hapa Dodoma, lakini tunaahidi kuwa na sisi tutahamia kwa awamu kama ambavyo Serikali imekuwa ikifanya. Hili litategemea upatikanaji wa viwanja na majengo kwa ajili ya ofisi, kwa hiyo wafanyakazi wetu nao watahamia taratibu,” alisema.
Post Views: 279