Na WAF – Dar es Salaam

Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama akikagua mabanda ya hospitali maalum zilizotengwa kwa ajili ya kuhudumia wageni wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati (Africa Energy Summit) unaofanyika kwa siku mbili katika Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 27-28 Januari, 2025.

Hospitali hizo ni pamoja na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) pamoja na Hospitali ya Aga Khan.

Wageni watakao hudhuria Mkutano huo ni pamoja na Wakuu wa Nchi 25 na Makamu wa Rais, Mawaziri Wakuu na Naibu Mawaziri Wakuu 10 na kufanya idadi ya viongozi wa ngazi ya juu kufikia 35, hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kupokea idadi kubwa ya viongozi katika tukio moja. 

Mkutano huo ni mwendelezo wa matunda ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maono yake makubwa katika kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia kati ya Tanzania na mataifa mengine ambapo Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea kujitangaza barani Afrika na Duniani kwa ujumla.      

.