Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Jenista Mhagama akifurahia jambo na Mama Janeth Magufuli mjane wa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, mara baada ya kuwasilisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Mama Janeth Magufuli, alipoenda kumjulia hali nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.  
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama akiwasilisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa na Mama Janeth Magufuli, mjane wa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, alipoenda kumjulia hali nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama akiwasilisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Mama Asina Kawawa, mjane wa Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Rashid Mfaume Kawawa, alipoenda kumjulia hali nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama akimuaga Mama Asina Kawawa mjane wa Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Rashid Mfaume Kawawa alipoenda kumjulia hali nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.