Waziri wa ujenzi na Uchukuzi,Prof. Makame Mbarawa leo ametoa taarifa ya awali ya uchunguzi wa ajali ya ndege ya Precision iliyopata ajali Bukoba na kuua watu 19, ambapo ameeleza mambo mbalimbali yaliyobainika katika ripoti hiyo ya awali
Akisoma ripoti hiyo mbele ya vyombo vya habari leo Novemba 24, 2022 Waziri Mbarawa ameleza uchunguzi wa awali uliobainika katika ripoti hiyo kuwa ni pamoja na hali ya hewa kubadilika ghafla mda mfupi ndege hiyo ilipofika na kutaka kutua.
” hali ya hewa Bukoba iliripotiwa kuwa nzuri mpaka ilopofikia saa mbili na dakika ishirini asubuhi ambapo ilibadilika ghafla na mvua kuanza kunyesha ikiambatana na ngurumo za radi na upepo mkali na mawingu mazito na ukungu, ndege hiyo ikaingia katika anga la Bukoba saa mbili na dakika 25 asubuhi na kukuta hali ya hewa imebadilika dakika kadhaa zilizopita.” Amesema
“Ndege hiyo ilizunguka kwa takribani dakika 20 kwa kutarajia uwezekano wa hali ya hewa kubadilika na kuwa nzuri. Baadaye rubani aliamua alianza matayarisho ya kutua katika njia yakuruka na kutua ndege namba 31 kutoka uelekeo wa ziwa.” Amesema
Waziri Mbarawa amesema mashuhuda wa ajali walioukuwa kwenye ndege walionusurika walianza kuona uwaja wa ndenge mara tu ilipokuwa inakaribia kutua kabla ya kutua ziwani.
“Kutokana maelezo ya abiria walionusurika njia hiyo ilikuwa inaonekana yaani njia ya ndege mashuhuda hao walieleza waliona njia ya ndege kuruka na kutua kabla ya ndege pamoja na alama zake katika sehemu ya mwanzo wa njia kabla ya kugonga kwenye au kutua kwenye maji”
Aidha waziri ameeleza kuwa ripoti hiyo imebaini kuwa mhudumu na abiria ndiyo waliofungua mlango wa ndege hata hivyo wananchi waliokuwa maeneo ya karibu wakifanya shuguli za uvuvi walifika haraka kusaidia na kusisitiza kuwa ripoti hiyo haijamtaja mtu aliyehusika na uokozi kutoka nje au ndani ya ndege
“Mlango wa ndege ulifunguliwa na mhudumu wa ndege kwa msaada wa abiria hata hiyo ripoti ya uchunguzi imesema wananchi waliokuwa wanafanys kazi za shuguli za uvuvi jirani na eneo la ajali walifika ndani ya dakika tano mara baada ya ndege kuanguka hali hiyo ilisaidia kumpa ujasiri mhudumu wa ndege na abiria waliokuwa ndani ya ndege baada ya kuona nje ya ndege kuna unaweza kuwasaidia.” Amesema
Vilevile Waziri Mbarawa ameeleza ni kwa nini huduma ya uokoaji haikufanyika kwa haraka na kusababisha hatari kutokea kutokana na boti ya uokozi kuwa mbali na kufika wakati zoezi la uokoaji likiwa limekalika.
“Tunayo boati ya uokozi katika ziwa Vikto wakati ajali hii inatokea boti hii ilikuwa kwenye doria kwenye maeneo ambayo ni mbali na ulipo uwanja wa Bukoba ikiwa katika kutekeleza majukumu yake ya kawaida ya doria, kwa vile ilikuwepo mbali ya eneo la uwanja wa ndege.
Kutokana na umbali huo boti hii ilipofika eneo la ajali shughuli za kuokoa watu zilikuwa zimekamilika”Amesema
Ripoti ya ajali ya ndege ya Precision iliyotokea Novemba 6, 2022 mita chache kutoka uwanja wa ndege wa Bukoba na kuua watu 19 na kujeruhi wengine 24 ni ya awali kama ilivyoahidiwa kutolewa ndani ya siku 14 baada ya kikao cha mawaziri kilichofanyika Dodoma, aidha ripoti kamili inatarajiwa kukamilika ndani ya miezi kumi na mbili