Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimpokea Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Filippo Grandi mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Agosti 24, 2022. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimsikiliza Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, Mahoua Parums, baada ya kumpokea Kamishna Mkuu wa Shirika hilo, Filippo Grandi (katikati), Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Agosti 24, 2022
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, Mahoua Parums, wakati walipokuwa wanamsubiri kumpokea Kamishna Mkuu wa Shirika hilo, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Agosti 24, 2022
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama, walipokutana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Agosti 24, 2022.