Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amepokea taarifa maalumu ya mapendekezo ya aina ya michoro ya vazi la Taifa kutoka kwa kamati iliyoundwa kwa ajili ya maandalizi ya vazi hilo.
Waziri Kabudi amesema mchakato wa vazi la Taifa umeanza kuwa na mafanikio kutokana na hatua zilizofikiwa kwa sasa ambapo kamati imewasilisha taarifa maalumu ya mapendekezo ya aina ya michoro ya vazi la Taifa kwa Wizara yake.
Kabudi ameyasema hayo Januari 9, 2025 jijini Dar es salaam wakati akipokea taarifa hiyo maalumu ya mapendekezo ya aina ya michoro ya vazi la Taifa kutoka kwa kamati maalumu ya uandaaji wa vazi hilo.
Kabudi amesema, ili kupata vazi la Taifa ni mchakatu wenye hatua tofauti na sio suala la mara moja bali ni lazima lipate maoni ya wananchi na wadau mbalimbali ambapo michoro hiyo iloyopendekezwa itachapishwa ili kila mmoja aione na atoe maoni yake.