Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa leo ametembelea ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zilizoko jijini Dar es Salaam.

Amepokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabir Kuwe.

Waziri Silaa amefanya ziara hiyo kwa lengo la kujifunza na kupitishwa kwenye majukumu yanayotekelezwa na mamlaka hiyo na namna wanavyoshughulikia masuala ya Habari na Mawasiliano.

Katika ziara hiyo, Waziri Silaa ameongozana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Nicholaus Merinyo Mkapa pamoja na Maafisa Waandamizi wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Waziri Silaa aliapishwa Julai 26, 2024 kushika wadhifa huo akichukua nafasi ya Nape Nnauye.