Waziri wa ulinzi wa Israel, Israel Katz ameapa kuzidisha mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza ikiwa kundi la wanamgambo wa Hamas halitoacha kurusha maroketi kuelekea Israel.
Waziri wa ulinzi wa Israel, Israel Katz ameapa kuzidisha mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza ikiwa kundi la wanamgambo wa Hamas halitoacha kurusha maroketi kuelekea Israel.
Gatz alisema ikiwa kundi la Hamas halitoruhusu kuachiliwa mateka wanaoshikiliwa katika Ukanda wa Gaza, watakabiliwa na mashambulizi makubwa ambayo hayajashuhudiwa kwa muda mrefu.
Waziri Katz, alitoa kauli hiyo wakati alipotembelea mji wa Netivot ulioko karibu kilometa 16 mashariki mwa Palestina.Jeshi la Israel lateketeza hospitali ya Gaza kwa moto
Hapo awali, jeshi la Israel IDF lilichapisha ujumbe katika ukurasa wa X likisema kwamba kundi la Hamas, lilifyatua roketi mbili katika mji huo wakati wa mkesha wa mwaka mpya.
Katz aliteuliwa kuwa waziri wa ulinzi mwezi Novemba baada ya mtangulizi wake Yoav Gallant kufutwa kazi kufuatia tofauti na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.