Na Lookman Miraji,JamhuriMedia, Dar es Salam

Siku ya Novemba 11 kila mwaka inatambulika kama siku maalumu ya kuwakumbuka mashujaa waliopoteza maisha katika vita vya kwanza vya dunia.

Historia inatueleza kuwa mnamo Novemba 11 ya mwaka 1918 wakati vita vya kwanza vya dunia vikiendelea, viongozi wawakilishi wa mataifa yaliyoshiriki katika vita hivyo wakiongozwa na wawakilishi kutoka nchi ya Ujerumani pamoja na Uingereza walikutana kwa majadiliano na mwishowe kutia saini ya hati ya kusimamisha mapigano yaliyosababisha vifo kwa mamilioni ya watu.

Mara baada majadiliano na utiwaji saini wa hati baina ya serikali hizo mbili vyombo na vyanzo mbalimbali vikaripoti kuwa ndiyo mwisho wa vita kuu ya kwanza vya dunia.

Hivyo mara baada ya hatua hiyo ndipo tarehe 11 ya mwezi wa 11 ikabaki kukumbukwa kama tarehe ya kumalizika kwa vita kuu ya dunia.

Maadhimisho ya siku hiyo huadhimishwa kila ifikapo tarehe novemba 11 duniani katika nchi wanachama za umoja wa madola kwa kuwakumbuka wale wote waliopoteza maisha katika vita hivyo.

Siku hiyo huadhimishwa ikiambatana na matukio matukio mbalimbali ikiwemo kuweka mashada ya maua kwenye makaburi ya wanajeshi wasiojulikana.

Kwa nchini Tanzania maadhimisho ya siku hiyo yameandaliwa na ubalozi wa Uingereza kwa kushirikiana na ubalozi wa Ujerumani yamefanyika leo hii jumapili ya Novemba 10, 2024 jijini Dar es salaam.

Mabalozi wa mataifa mbalimbali nchini kwa pamoja waliongozwa na Waziri wa maliasili na utalii, Balozi Pindi Chana aliyemuwakilisha waziri wa mambo ya nje, Balozi Mahmoud Thabit Kombo aliyetarajiwa kuwa mgeni rasmi katika shughuli hizo.

Akizungumza katika shughuli hizo balozi Pindi Chana amesema kuwa siku hiyo ni siku muhimu ya kuthamini na kujivunia hatua zilizochukuliwa na mashujaa hao waliopita katika kupigania uhuru na amani kwa wakati huo.

“Tunakusanyika leo kuadhimisha ushujaa wa nguvu za ajabu za wale waliokuja mbele yetu, wale waliotutumikia na wale wanaoendelea kuhudumu kwao. Watu hawa walisimama bega kwa bega kulinda maadili ya uhuru, utu na ubinadamu.

“Dhahabu zao zinalingana na wakati, ukumbusho mzito wa bei iliyolipwa kwa amani na uhuru tunaofurahia leo” Alisema.

Aidha balozi Pindi Chana amegusia juu ya vita zinazoendelea katika baadhi ya mataifa na kuomba jumuiya ya kimataifa kuzidisha juhudi za kuleta maazio ya amani.

“Hata hivyo, hata tunaposherehekea amani ya Tanzania, tunajali pia ukweli mbaya kuwa kwenye migogoro na vita vinaendelea kusumbua ulimwengu wetu.


Kuanzia mizozo ya muda mrefu hadi kuongezeka kwa hivi majuzi kama vile Migogoro ya Ukrainia ya Urusi, mzozo wa Hamas wa Israel, migogoro ya Somalia na sehemu ya mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kutaja tu machache ambayo yanatumia mateso na ugumu wa maisha usioelezeka kwa mamilioni ya watu.”

” Leo, tunapokumbuka dhabihu za zamani, lazima pia tukabiliane na changamoto za sasa kwa moyo wa moyo na kujitolea kwa amani. Tanzania imesimama kidete katika imani yake kwamba suluhu zenye ufanisi zaidi na za kudumu za migogoro na mtutu wa bunduki bali kidiplomasia na mazungumzo ya amani, tunaiomba jumuiya ya kimataifa kuzidisha juhudi za kuleta maazio ya amani ” Alisema.