Na Lookman Miraji, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Waziri wa ujenzi nnocent Bashungwa leo hii ameongoza hafla ya usainishwaji mikataba ya ujenzi wa daraja la jangwani, Dar es salaam.

Mkataba huo umesainiwa mbele ya viongozi mbalimbali wa kiserikali wa mkoa pamoja na wawakilishi kutoka TANROADS.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Bashungwa amesema kuwa ujenzi wa daraja hilo umegharimu takribani shillingi billioni 97.1 huku ikiwa ni sehemu ya mpango wa serikali katika kuboresha miundombinu.

Daraja hilo linategemewa kuwa na urefu wa mita 390 huku ikijumuisha barabara zenye maungio zenye mita 700 kila moja.

Aidha Waziri Bashungwa ameongeza pia kwa kusema kuwa serikali imetenga kiasi cha shillingi Billioni 125 katika kuhakikisha kuwa inakamilisha miradi yote inakamilika.

Miongoni mwa miradi hiyo iliyolengwa ni ujenzi wa daraja la kigogo, daraja la mkwajuni pamoja na kisarawe.

Mchakato wa ujenzi wa daraja la jangwani unatarajiwa kuchukua kipindi cha miaka miwili mpaka utakapokamilika.