Wazazi na Walezi wa Kijiji cha Tungamalenga Tarafa ya Idodi Wilaya ya Iringa mkoani Iringa wametakiwa kuacha tabia ya ulevi na kutotekeleza majukumu yao ya malezi kwa watoto ili kuhakikisha uliinzi na usalama wa watoto wao.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji hicho Afisa Tarafa ya Idodi, Makala Mapessah amesema kuwa kumekuwa na ongezeko la vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa kwa watoto wa kijiji cha Tungamalenga.

Mapessah amesema kuwa matukio ya ukatili kwa watoto katika Kijiji hicho yanachangiwa na wazazi na walezi kutumia muda mwingi kwenye kilimo cha Mpunga na Kuwaacha Watoto kwenye mazingira hatarishi kwa usalama Wao.

Ameema kuwa tatizo la ulevi kwa wazazi na walezi linatajwa kuchangia watoto kutelekezwa na kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo kwa kiasi kikumbwa vitendo hivyo huishia ngazi ya familia.

Mapessah amesema kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia vinatakiwa kutolewa taarifa kwa mamlaka zinazohusika ili kukomesha kabisa vitendo hivyo.

Alimalizia kwa kusema Kuwa Mkakati wa Serikali ya Tarafa na Kijiji cha Tungamalenga ni kuendelea kutoa elimu ya Malezi, Makuzi, Ulinzi na Usalama kwa Watoto Wenyewe, Wazazi na Walezi Pamoja na Jamii kwa ujumla.

Watoto wakisoma risala yao kwenye maadhimisho hayo wameitaka jamii na hasa wazazi kutopoka haki yao ya malezi na kuwaacha wakijilea wenyewe huku pia wakitaka hatua za kisheria kuchukuliwa kwa wanaotenda ukatili.

Please follow and like us:
Pin Share