Mwanafunzi mmoja amefyatua risasi katika shule ya binafsi ya Kikristo katika Jimbo la Wisconsin Marekani, na kujeruhi watu sita na kumuua mwalimu na mwanafunzi.

Mkuu wa Polisi wa Madison Shon Barnes alimtaja mshambuliaji huyo kuwa mwanafunzi wa kike mwenye umri wa miaka 15.

Mamlaka imesema mshambuliaji huyo alikuwa katika shule ya Abundant Life Christian School kabla ya kufyatua risasi na alikutwa amefariki katika eneo la tukio.

Wanafunzi sita walijeruhiwa, wakiwemo wawili waliopata majeraha yanayotishia uhai wa maisha yao.

Mwanafunzi wa gredi ya pili alikuwa wa kwanza kupiga simu, kwa mujibu wa Mkuu wa Polisi Barnes.

“Leo ni siku ya huzuni sio tu kwa Madison, kwa nchi yetu yote,” Barnes alisema.

Aliongeza kuwa polisi hawajabaini sababu za tukio hilo la ufyatuaji risasi, na familia ya mshukiwa ilikuwa ikishirikiana na uchunguzi.

Alisema bado haijabainika jinsi mshambuliaji huyo alipata bunduki.

Hata hivyo, matukio ya ufyatuaji risasi kwa wingi na wanawake ni nadra na ufyatuaji risasi shuleni unaofanywa na washambuliaji wa kike ni vigumu sana kutokea.