*Soma orodha uone maajabu, wamo masheikh, wachungaji

*Wengi wanatoka Dar es Salaam, Tanga, Zanzibar, Morogoro

*Mahakama yawaweka chini ya uangalizi, wanaripoti polisi

Majina ya Watanzania 255 wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya yamejulikana, na JAMHURI imeamua kuyachapisha. Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa kwenye orodha hiyo wamo watu maarufu na baadhi wamekuwa wakitoa misaada, huku wengine wakijifanya ni wazee wa kanisa na kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii.

Uchunguzi uliofanywa na JAMHURI, usio na chembe ya shaka, unaonesha kuwa orodha hii ya watu inayochapishwa hapa chini, kwa sasa wapo chini ya uangalizi wa Mahakama na Jeshi la Polisi nchini.

 

Watuhumiwa wengi ni wakazi wa Dar es Salaam, ingawa wamo wengine kutoka miji mikubwa ya Tanga, Zanzibar, Arusha na Morogoro. Aidha, idadi ya wanaume wanaoshiriki shughuli hiyo ndiyo kubwa.

 

Mkuu wa Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa, amethibitisha kuwa watu hao 255 ni kweli wamewekwa chini ya uangalizi wa Mahakama na Jeshi la Polisi.

 

“Ni kweli, kuna watu tumewapeleka mahakamani. Huko wanawekwa chini ya uangalizi, wanatakiwa waripoti kwa muda wanaopangiwa. Tunafanya hivyo baada ya uchunguzi wetu kubaini kuwa kweli wanahusika na biashara hii haramu,” amesema Nzowa.

 

Nzowa amegoma kutaja majina ya watu hao, lakini uchunguzi uliofanywa na JAMHURI kutoka ndani ya Jeshi la Polisi na katika Mahakama umefanikisha kupata orodha ya majina hayo.

 

Katika orodha hii, yumo Mchungaji aliyewekwa chini ya uangalizi, na baada ya kumaliza muda huo siku tatu baadaye akakamatwa na dawa nchini Brazil. Pia yumo Sheikh anayetoa misaada mbalimbali, lakini baada ya kukamatwa na dawa kilo 211 eneo la Kunduchi, Dar es Salaam, kwa sasa amekimbilia nchini Afrika Kusini. Huyu ni mkazi wa Sinza maarufu kama Shikumba.

 

Dawa zinavyoingizwa nchini

Hadi sasa kiwango kikubwa cha dawa za kulevya kinaingizwa nchini kwa njia ya meli katika Bahari ya Hindi. Baada ya meli kuwasili Tanzania, wasafirishaji hutumia boti ndogo ziendazo kasi kuchukua dawa hizo na kuziingiza nchini. Maeneo yanayotumiwa zaidi kuingiza dawa ni Bagamoyo, Zanzibar, Dar es Salaam, Tanga na Mtwara.

 

Jijini Dar es Salaam, boti hizo hutia nanga katika eneo la Bagamoyo ambako pia ndiko kwenye njia kuu ya uingizaji bidhaa za magendo zisizolipiwa kodi. Biashara hiyo huwahusisha baadhi ya polisi ambao mara kadhaa wamekuwa wakiwapa ulinzi wahalifu hao.

 

Viwanja vya ndege vinavyotumiwa kuingiza dawa za kulevya ni vya Julius Nyerere (Dar es Salaam ) na Abeid Amani Karume (Zanzibar ). Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) unaripotiwa kuwa na matukio ya nadra ya matukio hayo.

 

Taarifa kutoka Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya zinasema wasafirishaji wanaotumia ndege wamekuwa wakibuni mbinu mbalimbali, zikiwamo za kutumia manukato kwa ajili ya kuwapumbaza mbwa wenye mafunzo ya kubaini dawa za kulenya.

 

“Wanatumia perfume, wanatumia kahawa kupaka juu ya mifuko walimoweka dawa hizo. Mbwa wanaponusa wanashindwa kubaini dawa kwa sababu kunakuwa na harufu ya manukato au ya kahawa,” amesema mmoja wa maofisa wa kitengo hicho.

 

Habari zaidi zinasema kitengo kimepata vifaa maalum vya kubaini kama ndani ya mzigo kuna dawa za kulevya. Vifaa hivyo ni mfano wa sindano ambayo huchomwa kwenye mzigo na kuipitisha kwenye ngozi ya mwili, kama kuna dawa ikigusishwa kwenye ngozi unga unapukutika na kama mzigo hauna dawa za kulevya hakuna kinachotokea.

 

Tayari vifaa hivyo vimeanza kutumika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na vimefanikisha ukamataji wa magwiji wengi.

 

Ifuatayo ni orodha ya wauza unga ambao Mahakama imewaweka chini ya uangalizi, kwa maana kuwa wanaripoti polisi kila wiki kutia saini kwenye kitabu maalumu na kuthibitisha kuwa wamejirekebisha au wameacha tabia hiyo.

 

MAJINA YA WAUZA ‘UNGA’

1 Mwaija Hussein

2: Ally Omar Issa

3: Huruma Elnaja

4: Michael Stanley

5: Mabunduki Mapunda

6: Dunia Seleman

7: Justine Theophil

8: Abdallah Mfundo

9: Mashaka Bakari

10: Subira Bakari

11: Islama Rashid

12: Dickson Anthony

13: Gati Maginga Kilanga

14: Munira Khamis

15: Maul Said Kaikai

16: Athuman Moshi Kassimu

17: Mwajuma Mrisho

18: Maison John Mateso

19: Minyori Ramadhan Mohamed Kungulo

20: Khamis Kassim Juma

21: Simon Philipo Milanzi

22: Juma Khamis (a.k.a. Wakupotezea)

23: Ally Abdallah

24: Happy Zacharia

25: Iddy Athuman

26: Mohamed

27: Julius Paschal

28: Evod John

29: Haji Maneno

30: Omary Ally Bweka

31: Mohamed Omary Khatibu

32: Hashim Mohamed Pongwa

33: Hery Jaffar

34: Ahmed Shebe Ameran

35: Iddi Maulid Shaweji

36: Khamis Omary

37: Ramadhan Omary

38: Ismael Yusuf

39: Juma Rashid

40: Kuruthum Hamad

41: Zakaria Mohamed Sasamalo

42: Abdallah Mussa Mshindo

43: Mohamed Abdul Tindwa

44: Mohamed Hashim Masheli

45: Akida Ernest

46: Hassan Athuman Naheka

47: Salehe Mohamed Abdallah

48: Stumai Chande

49: Batuli Adam

50: Raymond Gilbert Jungulu

51: Adam Godwin

52: Zidi Mselem

53: Kassim Ally Juma

54: Dyamwale Chizenga

55: Abdallah Juma Reani

56: Habibu Waziri Kipawa

57: Abdul Mohamed Mwaurwe

58: Amanzi Said Amanzi

59: Salum Zarafi

60: Billy Sohal

61: Shukuru Peter

62: Omary Mfundo

63: Salehe Hemed

64: Said Ismail

65: Monica Kulanga

66: Charles Mrisho

67: Mwanaid Athuman

68: Bruno Msuya

69: Kassim Said

70: Denis Charles

71: Hassan Mhando

72: Aclesy Haule

73: Salum Yusuf Kimwaga

74: Abedi Mfundo

75: Tunu Said

76: Fatuma Salehe

77: Mwajuma Salehe

78: Salum Khamis

79: Mbwana Mbaraka Mkanga

80: Daud Ally Chambuso

81: Ibrahim Ramadhan Mniga

82: Rozi Lukasi

83: Udugu Jumbe

84: Mohamed Kalota

85: Godwin Vitus Chacha

86: Eliasa Athuman

87: Mvano Ova Hussein

88: Mood Dudufued

89: Issa Dachi

90: Filbert Swai

91: Hussein Francis

92: Mirambo Hassan

93: Nasibu Abdallah

94: Tariq Salim Abass

95: Omary Said Mumomo

96: Zuberi Mwamba Mabruki

97: Abdallah Haji Mrisho

98: Khamis Athuman Khamis

99: Vodika Roosevelt

100: Dotto Shabani Mohamed

101: Twaef Mohamed Ghanim

102: Salum Hamis Ramadhan

103: James Benezeti Munishi

104: Rahim Abdul

105: Juma Stumai

106: Luti Elias

107: James John

108: Hussein Mbwana

109: George Renatus Masalu

110: Jamal Rashid

111: Asha Thabiti

112: Zaituni Abdallah – Mama Sued

113: Fatuma Juma – Mama Simba

114: Salama Juma

115: Juma Jamali

116: Juma Mussa

117: Abdulrahman Mbaraka

118: Maneno Said Kitungi

119: Mussa Salum

120: Hashim Ashirafu

121: Nyambuya Joel

122: Rashid Burhani Milanzi

123: Ally Mikidadi Ngunde

124: Mwijuma Ibrahim Kondo

125: Halifa Said

126: Shaban Said Makuka

127: Khamis Ramadhani Mgomba

128: Ruzuna Mwakasha

129: Rajabu Mohamed (Roger)

130: Athuman Chande

131: Shamin Azizi

132: Hashim Hashid Mashaka

133: Hussein Hamis

134: Ibrahim Rajabu

135: Mohamed Rajabu Mkali

136: Hatim Cheucheu Hungu

137: Hamis Uyoro (Kikoti)

138: Seif Hassan

139: Mnyamisi Mungia Khamis

140: Said Kisoka Said

141: Bakari Suleiman

142: Mwaita Mohamed

143: Asubisye Mwasumbi

144: Dalmat Jovin

145: Ally Rashid Dilunga

146: Mwinyi Seleman Mwachuo

147: Zinduna Ramadhan

148: Sanky Seleman (a.k.a Nzowa)

149: Karume Ngoi (a.k.a Karume)

150: Issa Thabit

151: Victor Patrick

152: Kiteguo Seif Ndumbikwa

153: Mbwana Mohamed (Liyobo)

154: Bonifasi Kulanga

155: Kidunda Omary

156: Amani Mavula

157: Mchola Bakari Majomba

158: Mohamed Simba Kassim

159: Asha Yusufu (Rasta)

160: Mshamu Njanga Abdallah

161: Zena Selemani Mwanaisha Abdallah

162: Ally Abdallah Pashua

163: Mbaruku Rashid Rajabu

164: Mohamed Jumbe Mohamed

165: Seleman Mohamed Masoud

166: Kabote Mfaume Kiboko

167: Selehe Hemed Lugongo

168: Muharami Mohamed Abdallah

169: Hatibu Nyamisi Nyangasa

170: Juma Alfan Hussein

171: Khariri Mohamed Khariri

172: Alfreda Anjelo Kulanga

173: Elly Hamis Mrisho

174: Iddi Haji Fumo

175: Ras Juma Ally

176: Ally Khatibu Haji

177: Hemed Juma Mrisho

178: Abdallah Hamza Said

179: Mohamed Noor Sheikh

180: Selemani Omary Zuberi

181: Hassan Masoud Ally

182: Akida Ayubu Akida

183: Bakari Abdurahman Bakari

184: Bashiri Mohamed Shallie

185: Jamal Rashid Ismail Mkoko

186: Ally Juma Said

187: Pili Ramadhani

188: Mosses Lwama

189: Mbaraka Shaban Muba

190: Richard Mbunda

191: Ayubu Mfaume Kiboko

192: Abbas Mohamed Hussein

193: Juma Hemed Tumbo

194: Sophia Joseph Ntembo

195: Said Hilal Abdallah

196: Thabit Juma Khamis

197: Suleman Bakari

198: Salum Abasi

199: Mustafa Omary Mwinyi

200: Alim Iddi Said Mwinyi

201: Othman Juma Othman

202: Shaban Kibwana Seif

203: Raymond Swift Mwakatwila

204: Abas Bachu Kasu

205: Jumanne Ramadhan Chambala

206: Irene Godfrey Mhina

207: Abdallah Abdurahman (Kidagaa)

208: Uwesu Ally Hussein

209: Zuberi Ally Mohamed

210: Khamis Seleman Khamis

211: Said Seleman Khamis

212: Mwarabu Bakari Mwarabu

213: Rajabu Shaban Juma

214: Ally Mohamed Seif

215: Mohamed Hassan Mkachika

216: Ally Bakari Mloli

217: Kelvin Daud Mchikinyi

218: Ally Mohamed Nyundo

219: Fatuma Juma (Mama Simba)

220: Shukuru Thabit Mtetwa

221: Mshamu Mjanga Abdallah

222: Zena Seleman (Mwanaisha Abdallah)

223: Ally Abdallah Pashua

224: Mbaruku Rashid Rajabu

225: Eliud Juma Mbwambo

226: James Patrick Mwangi

227: Hemed Abdallah Mwinyimvua

228: Juma Said Hussein

229: Haidery Mohamed

230: John Kauta

231: Mohamed Salehe

232: Doreen Josephat Urio

233: Richard Barnabas Mfundo

234: Soud Awadhi Mzee

235: Maneno Rajabu

236: Mdanzi Mjaja

237: Khalid Ramadhan

238: Soud Rasheed Soud

239: Issa Mangara Seid

240: Omary Salehe

241: Omary Ramadhan Yusuf

242: Mfaume Said Mugulo

243: Ramadhan Miraji Mkangata

244: Abdallah Nassoro Kimoko

245: 0mary Juma Mohamed

246: Ally Said Omary

247: Abdallah Nassoro (Kibwetere)

248: Mariam Yona M’ngata

249: Hussein Mohamed Hariri

250: Tom Juma Masoud

251: Frank Obed Shoo

252: Jaffar Kassim Jaffar

253: Karume Ngoi

254: Adamu Mohamed Monde

255: Liliani Kimei