Wahamiaji haramu na walowezi wanaoishi hapa nchini wanatumia mwanya wa usajili wa laini za simu wa ‘mwendokasi’ kujipatia vitambulisho vya taifa, JAMHURI limebaini.
Hali hiyo imeelezwa kuwapo katika mikoa ya pembezoni mwa nchi, na tayari malalamiko kadhaa yamekwisha kupelekwa kwenye mamlaka husika. Miongoni mwa maeneo yanayotajwa kukumbwa na hali hiyo ni wilaya za Longido na Ngorongoro.
“Sisi hapa Ngorongoro hali hiyo ipo kwa sababu hata wale waliokuwa blacklisted wakazuiwa kupewa vitambulisho vya mpiga kura, sasa wamepewa vitambulisho vya taifa,” kinasema chanzo chetu.
Imeelezwa kuwa hata viongozi waandamizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika ngazi ya wilaya na Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro ambao walinyimwa haki za uraia kwa vile ni walowezi kutoka nchi jirani, baadhi yao wamepata vitambulisho kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Hali hiyo imemfanya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, acharuke na kutoa maagizo kwa wahusika.
Akizungumza na JAMHURI, Lugola anasema: “Najua wapo wanaotumia fursa hii ya msongamano wa kusajili laini za simu kwa ajili ya kupata vitambulisho vya uraia. Nawaonya waache mara moja.
“Wanaona watu tuna presha ya kusajili laini wao wanapenya, ninatoa mwito kwa wananchi wote kuwa macho. Ulinzi wa taifa letu ni wa vyombo vya ulinzi na usalama na wananchi wote wenye mapenzi mema.
“Natoa rai kwa kila mwananchi kuwa makini kwa kutoa taarifa kwenye vyombo husika pale wanapoona au wanapoambiwa kuna mtu au watu wasiokuwa raia wanaopenya na kupata ‘uraia’ kwa njia za mkato.
“Kila mwananchi asisite kutoa taarifa ya maandishi, ya mdomo au kuweka pingamizi kwa mhamiaji haramu yeyote anayepata kitambulisho cha taifa. Wenye taarifa za watu hao wanaweza kutuletea kwa njia ya siri na sisi tutahifadhi siri hizo na wala majina yao hayatatangazwa au kujulikana,” anasema.
Waziri Lugola anasema ni rahisi zaidi kwa wananchi kuwabaini wahamiaji haramu wanaojipatia uraia kwa kuwa wanaishi nao.
“Wananchi wanakaa nao, wanawajua. Kila Mtanzania awe na uchungu na nchi yetu, maana bila hivyo tunaweza kujikuta tunakuwa na wageni wengi wanaojipatia uraia kwa njia haramu,” anasema.
Kuhusu ukubwa wa tatizo hilo mkoani Arusha, hasa katika maeneo ya Longido na Ngorongoro, Waziri Lugola anasema: “Maeneo ya pembezoni yana changamoto nyingi, na hilo la baadhi ya wageni kuja nchini na kuwa viongozi, naamini Uhamiaji watalishughulikia kwa mujibu wa sheria.”
Katika hatua nyingine, waziri huyo anasema kazi ya utoaji vitambulisho na uandikishaji wa laini za simu inayoendelea hailengi kuwakomoa wananchi, bali inalenga kuleta tija zaidi kwa nchi na wananchi.
“Hakuna nchi inataka kuwaumiza au kuwakomoa wananchi wake, huu ni mfumo mzuri sana wa usalama wa watu na nchi yetu. Wananchi wasichukulie kuwa hii ni kero. Usajili wa laini za simu pamoja na vitambulisho vya NIDA vitasaidia mambo mengi sana kwenye usalama na kichumi. Tutajua nani ni nani, yuko wapi na anafanya nini. Wahalifu watabanwa vizuri zaidi na kero nyingine kama za kudaiwa barua za watendaji zitapungua kwa kuwa na kitambulisho cha NIDA. Wananchi wasione kuwa serikali inawakomoa. Kama laini imefungwa ni kwa muda tu na baada ya usajili mwananchi anaweza kurejesha laini yake ile ile au akiamua anapata nyingine,” anasema Lugola.
Mmoja wa viongozi waandamizi wa Idara ya Uhamiaji mkoani Arusha amezungumza na JAMHURI na kueleza kuwa pamoja na changamoto za usajili wa laini za simu, wamejitahidi kuhakikisha hakuna mlowezi au mhamiaji haramu anayepata kitambulisho cha uraia cha NIDA.
Akizungumza kwa masharti ya kutotajwa jina, anasema: “Kweli Ngorongoro kuna rejesta ya wahamiaji haramu na walowezi. Nadhani idadi ni kama 250 hivi, hao wanajulikana na kwa kweli tumehakikisha hawapati vitambulisho vya uraia. Majina yao yameingizwa kwenye system (mfumo) kiasi kwamba jina likionekana tu tunapata taarifa.
“Fomu zote za maombi ya vitambulisho tunazipitia na sharti zisainiwe, na kila anayeandikishwa tunapitia taarifa zake na kuzipitia kwa mtu mmoja baada ya mwingine – kwa hiyo nikuhakikishie kuwa kama yupo aliyepenya, tutampata,” anasema.
Ofisi hiyo ya Uhamiaji Mkoa inasema miongoni mwa wanaochunguzwa uraia wao ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ngorongoro, Ndilango Senge.
Katika Kijiji cha Ololosokwan, Tarafa ya Loliondo, Ngorongoro, raia wa Kenya, Esophio Parmwat; licha ya kubainika kuwa si raia wa Tanzania, aliwania uenyekiti wa serikali ya kijiji hicho.
Idara ya Uhamiaji Wilaya ya Ngorongoro katika barua yake kwenda kwa Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo, ilisema kuwa Parmwat si raia wa Tanzania, na kwa sababu hiyo hapaswi kuwania nafasi yoyote ya uongozi.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ngorongoro, Roza Kiromo, licha ya kushika wadhifa huo, yuko kwenye orodha ya watu ambao uraia wao una shaka.
Orodha ya walowezi wanaoishi Loliondo
Katika vijiji kadhaa katika Tarafa ya Loliondo kumepatikana majina 224 ya ‘Wakenya’ ambao, ama ni wahamiaji haramu, au walowezi. Wanaishi na kuendesha shughuli zao huku wakipata haki zote kama Watanzania.
Uchunguzi uliofanywa na JAMHURI umebaini kuwa miongoni mwa walowezi hao ambao uraia wao unatiliwa shaka, tayari wamekwisha kupata vitambulisho vya NIDA kama raia halali, na si walowezi. Hali hiyo inakinzana na taarifa ya Uhamiaji Mkoa wa Arusha. Ifuatayo ni orodha iliyoandaliwa miaka kadhaa iliyopita:
1: Peter Kiromo
2: Elizabeth Nairushiye
3: Kennedy Manyeki
4: Katikasha Kamanga
5: Risa Kamanga
6: Huho Daniel
7: Jackson Manyeki
8: Glady Kurgat
9: Elizabeth Ongetont
10: James Koromo
11: John Nzuna
12: Anna Ramasigonde
13: Omaria Lengaaki
14: Nangaya Lengaaki
15: Ndito Lengaaki
16: Kalee Saitabau
17: Najara Koleli
18: Joshua Saitabau
19: Timan Rika Yion
20: Ngopeesho Olekorkai
21: Ngisu Olenanyokie
22: Joel Siyianga
23: Sikemboi Sisi
24: Noosokono Koleli
25: Lasaru Saitabau
26: Noorkorea Sisi
27: Olemeen Ngoikor
28: Joel Lengaaki
29: Elija ole Matian
30: Joel Siyanka
31: Parkipoi Murera
32: Iman Olemetian
33: Nangida Olemen
34: Joshua Mwarabu
35: Oloibor Ngapai
36: Andrew Nkanuma
37: Sintako Nkanuma
38: Ngaina Saitabau
39: Nosilat Naingisa
40: Susana Massago (mama)
41: Binifas Massago
42: Oloongoshoka Ndaiya
43: Lengoko Saitabau
44: Modolu Yengo
45: Sirere Mpoe
46: Oleengot Engo
47: Oletimoi Stephen
48: Joshua Marabui
49: David Sais
50: Lekakiuy Sananka
51: James Massago
52: Bebi Massago
53: John Ngile
54: Ole Kileu
55: Ole Sasii
56: Joel Karori
57: Chuma Shambarao
58: Olooseenge Rea
59: Sakaria Narikai
60: Orandaya Kitipa
61: Alex David
62: Dopoi Kitipa
63: Kosia David
64: Porosooi Ndaiya
65: Boma ya Oleshung
66: Boma ya ole Serei-Kututuo
67: Boma ya Olekitipa
68: Nganuma Lemorara
69: Nganeni Lemorara
70: Ng’onene Nkanuma
71: Anna Gathu
72: Ruth Kabulunze Musomba
73: David Marko Sessat
74: Naomi Marko Sessat
75: Josephine Kuria
76: Joseph Kabulunze Musomba
77: Elizabeth Musumba
78: Marco Muhinge
79: Christine Musomba
80: Ndolee Temwee
81: Jane Koromo
82: Philipo Justus Marco
83: Pareyo Kitipa
84: Olengutie Saing’eu
85: Lekinyit Reyia
86: Esophie Parmat na ndugu zake
87: Kararit Ndaiya
88: Peter Kashal
89: Olemundere
90: Kisarunga Leitura
91: Luthia Ngelenche
92: Christine Francis William
93: Christopher Marco Sessat
94: Denis Okirigiti
95: Aizack Tura
96: Magreth Kiromo
97: Peter Robert Kiromo
98: Steven Kabulunje (dereva Hifadhini)
99: Peter Mtune Kaput
100: John ole Keroto
101: Siminde Lonyori
102: Anna Ngelenche
103: Zakayo Sesat
104: Pius Mtune Kaput
105: Emmanuel Samwel
106: Joseph Sessat
107: Estomih Manyeki
108: Joachim Manyeki
109: Felomona Mtune Kaput
110: Godfrey Kiromo
111: Godwin Mtune Kaput (Mwalimu Halmashauri)
112: Lazaro Sessat
113: Beatrice Kimoro
114: Evaline Bilechi
115: Saimon Sessat
116: Emmanuel Sassat
117: Lucy Chambii
118: George Mtune Kaput
119: Yasinta Dunya
120: Anna Cheburge
121: Joyce Marko
122: Elizabeth Robert
123: Mamiam Koira
124: Lilian John
125: Josephine Koillah
126: Sananga Cooss
127: William Sangupa
128: Coos
129: Olekoreko
130: Amos Olekoreko
131: Joseph Olekoreko
132: Joseph Sessat
133: Mery Kuyato
134: Joseph Kipkia
135: Gudito Nyange
136: Marco William Mabwa
137: Yeremia Olekoreko
138: Napirura Olengopiri
139: Mapena Olengopiri
140: Manina Olenanyika
141: Kiparian Manina
142: Emmanuel Mtune Kaput
143: Nayeilo Angangi
144: Ndina Manina
145: Moris Manina
146: Soinkei Olekumbe
147: Naaramataki Olekumbe
148: Saaloi Leshashi
149: Langoi Leshashi
150: Sabina James Kiromo
151: Rozi Kiromo
152: Lourence Kiromo
153: Emmanuel Kiromo
154: Ateiti Sumare
155: Orkedienye Kapiro
156: Saruni Ngurumwa
157: Sanare Koshara
158: Kisoku Karbolu
159: Memus Sadira
160: Nanjiko Shukur
161: Kipuri Karbolo
162: Nginandei Melejeki
163: Makoi Melejeki
164: Kanaya Karbolo
165: Napatao Meyane
166: Maripet Purengei
167: Oloishuro Kariro
168: Oleshololoi
169: Kingorosh Manatiny
170: Frank Mtune Kaput
171: Kanai Mbatiany
172: Kashing Pikoyan
173: Naingei Koikay
174: Simore Letuluko
175: Nareyo Olekandika
176: Oleniboo
177: Michael Kitipa
178: Kayo Kitipa
179: Korema Mako
180: Shukuru
181: Olonyikid Sironike
182: Olokose Kapiro
183: Karungu
184: Moriko Ngurumwa
185: Shinga Mboe
186: Olorupa Pere
187: Sangau Mbatiany
188: Kararinyayia
189: Olesironik
190: Molinge Oloso
191: Orkelese Ndaiya
192: Ntumaini Nkanuma
193: Nteetu Nkanuma
194: Kosiando Tuke
195: Sopiya Kosiando
196: Daudi Mtune Kaput
197: Juliana Mtune Kaput
198: Francis Mabwa
199: Yohana Sessat
200: Saitoti Kosiando
201: Tina Leshana
202: Shirimu Kuya
203: Ndooriti Koleli
204: Ngicha Oleneko
205: Musu Ngicha
206: Lonyokie Ngicha
207: Tiene Ngicha
208: Titio Ngicha
209: John Kamanga
210: Mbizi Ololeng’a
211: Olengaiki Olepombo
212: Joseph Siere
213: Melejeki Olemunya
214: Saitoti Ngekee
215: Lesidai Melejeki
216: Koika Melejeki
217: Mbaayi Kosiando
218: Ndima Kosiando
219: Koleli Lesite
220: John Koleli
221: Kijooli Melejeki
222: Esophip Parmwat
223: Marco Parmwat
224: Kunday Parmwat