Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema kwa kushirikana na Ofisi ya Taifa ya Mashitaka limewafikisha mahakamani watuhumiwa 270 kwa makosa ya ubakaji na watuhumiwa wawili kati yao wamefungwa kifungo cha maisha jela na wengine miaka thelathini kila mmoja.
Akitoa taarifa hiyo hii leo Desemba 14,2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishina Msadizi wa Polisi ACP Justine Masejo amesema kati ya watuhumiwa 270 watuhumiwa 223 walipatikana na hatia kati yao wawili ambao ni ni Peter Leonard (27), mkazi wa Lashaine Monduli kwa kosa la kubaka mtoto mwenye (7) na Paul Hilonga (60) ,mkazi wa Karatu wote wawili wamefungwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kubaka.
Kamanda Masejo amewaambia waandishi wa habari kuwa Jeshi hilo liliendesha operesheni maaalum ambapo watuhuiwa 127 na pikipiki 125 zilikamatwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo za taa ambazo zimepigwa marufuku,makosa mengine ni kuwa na namba bandia,pamoja na pikipiki ambazo zimefutwa namba.
Ameongeza kuwa pikipiki hizo zimekuwa kero kwa wananchi husasani wenye magonjwa mbalimbali nak ubainisha kuwa jeshi hilo linaendelea na msako mkali wa vyombo hivyo ambapo amesema wanafanya utaratibu wa kimahakama kutaifisha pikipiki hizo.
ACP Masejo alitoa rai kwa wananchi wa mkoa huo kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ili kukomesha vitendo vya kihalifu pia amebainisha kuwa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama wamejipanga vyema sikukuu za mwisho wa mwaka.
Kwa upande wake Juma Buruani alisema wao kama viongozi wa waendesha pikipiki wataendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi na kutoa rai kwa wenza kuachana na vitendo ambavyo vitawafanya kukamatwa na jeshi hilo.
Mwenyekiti wa waendesha pikipiki kutoka kata ya Murieti alisema kuwa wataendelea kutoa elimu kwa madereva wenzao ili kuwa na uelewa wa pamoja.