Jeshi la Polisi nchini kupitia kitengo cha Kuzuia na Kupambana na dawa za kulevya (Anti Drug Unit) “ADU” kwa kushirikiana na Polisi mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani limefanya operesheni, doria na misako iliyofanyika katika maeneo mbalimbali hapa nchini nakufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wa madawa hayo.
Katika kipindi cha Mwezi Julal hadi Novemba, 2022. jumla ya kesi 369 zilifikishwa mahakani na kutolewa maamuzi hapa nchini ambapo watuhumiwa 377 walitiwa hatiani. Watuhum iwa 170 walifungwa vifungo mbalimbali na 207 wamelipa faini na kuachiwa huru. Vile vile vyombo vya moto (Magari 8. Pikipiki 9, Boti 02) na Nyumba O1 vilitaifishwa na Mahakama kuwa Mali za Serikali.
Aidha Jeshi la Polisi Nchini linaendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya madhara ya utumiaji wa madawa ya kulevya katika maeneo mbalimbali ikiwemo nyumba za ibada, masoko, vituo vya mabasi, maeneo burudani na kwenye mikusanyiko ya watu.
Sambamba na hilo Kitengo cha Kuzua na kupambana na dawa ya kulevya (ADU) kwa kushirikiana na wadau pamoja na Taasisi za kimataifa tunaendelea kufanya warsha mbalimbali katika kubaini, kujadili na kupanga mikakati ya kupambana na dawa za kulevya Nchini.
Jeshi la Polisi Nchini linatoa wito kwa wananchi kuwa halito muonea muhali mtu yeyote atakae kamatwa akijihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya na linawaomba wananchi kutoa taarifa za watu wachache wanaojihusisha na matukio ya uhalifu ili hatua zichukuliwe dhidi yao.
Pia linawataka wamiliki wa vyombo vya moto kusimamia vyombo vyao muda wote ili kuepuka kupata hasara pindi vitakapo kamatwa vikitum ika katika kusafirisha dawa za kulevya.
Mwisho tunashukuru vyombo vya Habari katika kuendelea kutoa elimu juu ya athari zitokanazo na dawa za kulevya. kwa ujumla zina athiri nguvu kazi ya Taifa.