Na Magrethy Katengu,JamuhuriMedia, Dar es Salaam
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevyab(DCEA) imewatia mbaroni watuhumiwa 21 kwa kuhusika na za dawa za kulevya jumla ya Kilogramu 767.2 ikiwemo aina ya heroin, methamphetamine, na skanka .
Ukamataji huo wa watuhumiwa hao ni operesheni ikiyofanyika kuanzia Aprili 4hadi 18 ,2024 katika Mlmikoa ikiwemo Tanga, Pwani na Dar es Salaam na kufanikiwa kunasa dawa hizo na watuhumiwa.
Akizungumza leo Aprili 22 ,2024 na Waandishi wa habari lJijini Dar es salaam Kamisha Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na dawa za kulevya (DCEA) Aretas Lyimo amesema kati ya dawa zilizokamatwa,heroin ni Kilogramu 233.2, methamphetamine kilogramu 525.67 na skanka Kilogramu8.33 .
Kamishna amebainisha kuwa Operesheni iliyofanyika Aprili 4,2014 walifanikiwa katika eneo la Mikwanjuni Jijini Tanga ambapo watuhumiwa wawili walikamatwa wakiwa na dawa za kulevya aina ya heroin kiasi cha gramu 329.412 na Aprili 8 mwaka huu eneo la Wailes Temeke mtaa wa Jeshini Jijini Dae rs salaam watuhumiwa wawili walikamatwa kuhusika na dawa za skanka kilogramu 1.49 .
Pia Katika Operesheni ikiyofanyika Aprili 10 mwaka huu eneo la Zinga Bagamoyo Mkoani Pwani dawa za kulevya Metamphetamine kilogramu 424.84 huku watuhumiwa watatu walikamatwa kuhusika na dawa hizo na tarehe hiyo hiyo katia eneo la Kunduchi Jijini Dar es salaam alikamatwa mtuhumiwa mmoja akiwa na dawa za kulevya aina ya heroin kiasi cha gramu 158.24 na Aprili 14 ,2024 eneo la bandari Jijini Dar es salaam zilikamatwa kilogramu 4.72 dawa aina ya skanka na watuhumiwa watatu walikamatwa kuhusika na dawa hizo
Sanjari na ukamataji huo zoezi liliendelea ambapo Aprili 16,2024 katika kata ya Kunduchi Jijini Dar es salaam zilikamatwa kilogramu 232.69 za dawa za kulevya aina ya heroin na kilogram 100.83 za dawa ya kulevya aina ya methamphetamine zilizokuwa zikiingizwa nchini kupitia bandari ya Hindi na watuhumiwa 9 walikamatwa katika tukio hilo pia Aprili 18,2024 Mtuhumiwa mmoja alikamatwa eneo la bandari Jijini Dar es salaam akiwa na kilogram 2.12 za skanka .
“Imaebainika mbinu mpya ya baadhi ya wafanyabishara wa dawa za kulevya wameendelea kutumia vifungashio vyenye majina ya aina mbalimbali ya kahawa na chai kama vile organic cocoa, na green tea kwa lengo la kukwepa kutiliwa mashaka wakati wa kusafirisha dawa hizo hivyo kwakuwa sisi tumejipanga vya kutosha kwa kupewa mafunzo na kuwa na nyenzo za kutosha tutahakikisha tunafanya doria ya kila mahali kidhibiti wimbi la wasafirishaji dawa za kulevya” amesema Kamishna
Aidha pia amebainisha kuwa baadhi ya boti za wavuvi wamaekuwa wakishirikiana na wafanyabishara hao kusafirisha dawa hizo hivyo wanaendelea na doria za kufuatilia boti zinazoendelea kujihusisha na usafirishaji dawa za kulevya na watawakamata hao wavuvi sheria kali zitachukuliwa dhidi yao ikiwemo kufikishwa mahakamani.
Hata hivyoa amesema kati ya watuhumiwa hao waliokamatwa wengi wao ni kundi la vijana na kundi hilo ikiwa litaendelea kujiingiza kwenye bishara na matumizi ya dawa za kulevya Taifa litapoteza nguvu kazi na hatimaye kuhatarisha uchumi na usalama wa Taifa letu.