MAMLAKA nchini Myanmar imesema leo kwamba tetemeko kubwa la ardhi limewaua zaidi ya watu 1,000 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 2,300 huku makumi ya wengine wakiwa hawajulikani walipo.

Mamlaka nchini Myanmar imesema leo kwamba tetemeko kubwa la ardhi limewaua zaidi ya watu 1,000 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 2,300 huku makumi ya wengine wakiwa hawajulikani walipo.

Myanamar ilipigwa na tetemeko hilo la ardhi la ukubwa wa kiwango cha 7.7 katika kipimo cha Richter. Mataifa mbalimbali duniani ikiwemo China, Malaysia na Urusi tayari zimetuma vikosi vya uokozi kwenda kutoa msaada.

Kiongozi wa timu ya uokozi ya China iliyotumwa nchini Myanmar, Wang Mo amesema ” timu hii ya uokoaji ina washiriki wenye ujuzi waliopewa kazi ya usimamizi, utafutaji na uokoaji, huduma za matibabu, na vifaa. Tunajivunia kushiriki katika misheni hii ya kimataifa ya uokoaji na tuna uhakika katika kukamilisha kazi zetu.”

Kwingineko katika nchi jirani ya Thailand iliyokumbwa na tetemeko hilo pia, watu sita wamefariki dunia na wengine 47 bado hawajulikani walipo.