Na Mwandishi Wetu

Watu sita wamefariki dunia na wawili kujeruhiwa katika ajali ya gari dogo la  abiria aina ya Toyota Hiace yenye namba za usajili T766 DQP iliyogongana uso  kwa uso na lori la mizigo wilayani Bukombe mkoani Geita.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo amethibitisha kutokea ajali hiyo  ambayo imetokea leo Julai 13,  2023 majira ya saa 11 alfajiri, eneo la Kata ya Runzewe, ambapo gari dogo ilikuwa ikitokea Kahama kwenda Ngara , huku lori likitoka Rwanda kuelekea Nairobi.

Amesema uchunguzi wa awali unaonyesha chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari ndogo,, Habibo  Abedi ambaye anadaiwa alisinzia, kisha kuacha njia na kwenda upande wa pili wa barabara.

Amesema wa gari hilo kubwa alifanya juhudi kuikwepa Hiace hiyo lakiniilikuwa katika mwendo kasi, hivyo kusababisha  vifo vya watu sita akiwemo dereva wa Hiace na kondakta wake.

“Majeruhi hali zao sio nzuri, walikuwa Kituo cha Afya cha Uyovu, na sasa hivi wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita,” amesema.