Kiongozi wa tawi la kijeshi la Hamas huko Gaza Mohammed Deif anaaminika kuwa miongoni mwa wahanga wa shambulizi la anga la Israel ambalo mamlaka ya afya inayoendeshwa na Hamas huko Gaza
Kiongozi wa tawi la kijeshi la Hamas huko Gaza Mohammed Deif anaaminika kuwa miongoni mwa wahanga wa shambulizi la anga la Israel ambalo mamlaka ya afya inayoendeshwa na Hamas huko Gaza imeripoti kuwa watu 71 wameuawa na mamia kujeruhiwa.
Gazeti la Haaretz la nchini Israel limesema vyanzo vya jeshi vinaamini kuwa kiongozi huyo wa al-Qassam Brigades aliuawa katika shambulio hilo.
Kwa upande wake, Jeshi la Ulinzi la Israeli (IDF) limesema kuwa shambulizi lilimlenga Deif na kiongozi mwingine wa kundi hilo katika mji wa Rafa Salama katikati ya Khan Younis. Ingawa bado hawajathibitisha iwapo viongozi hao wawili ambao wanatajwa kuwa walitengeneza mpango wa tukio la Oktoba 7 mwaka uliopita wamefariki.
Jeshi la Israel limesema lililenga eneo la Hamas na hakukuwa na watu katika eneo hilo kwa hivyo waathirika huenda pia wakawa ni wanachama wa kundi hilo ingawa ripoti za ndani ya Palestina zinadai kuwa shambulizi hilo limelenga makazi na mahema ya watu waliolazimika kuyakimbia makazi yao.