Takribani watu 30 wametangazwa kuwa hawajulikani walipo baada ya maporomoko ya ardhi katika kijiji cha Jinping kilichopo kusini-magharibi mwa China, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali ya China.
Maporomoko hayo ya ardhi yalitokea katika kijiji cha Jinping kilichopo mkoa wa Sichuan saa 11:50 kwa saa za hauko (03:50 GMT), yakifukia nyumba 10 na kuwazuia baadhi ya wakazi. Watu wawili walinusurika.
Kituo cha dharura kimeanzishwa kwenye eneo la tukio, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye ofisi ya usimamizi wa dharura ya wilaya hiyo.
Rais wa China Xi Jinping ameagiza “msako mkali kufanyika ili kuwanusuru watu wote wasiojulikana walipo” na hatua kuchukuliwa kwa wale waliokolewa.
Maelfu ya wafanyakazi wa dharura wanatafuta manusura, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Wizara ya Usimamizi wa Dharura ya China.